Friday, August 8, 2008

mayala aendelea vizuri
paschal mayala, mwandishi mwandamizi na mtangazaji aliyepatwa na ajali ya pikipiki akielekea dodoma wikiendi ilopita, anaendelea vyema katika hospitali ya muhimbili kitengo cha moi alikolazwa kwenye wodi J.
habari zilizagaa jijini kutwa nzima leo kwamba jamaa kavuta. nimeongea naye muda mfupi uliopita paschal akaniambia kwamba hata yeye kapata habari hizo kwamba amefariki, akisema huenda hiyo ruma ilisababishwa na yeye kuhamishiwa chumba kingine na kuna mdau aliyefikia chumba chake cha awali kukuta kitanda kitupi akajua tayari na kusambaza uvumi.
amesema anaendelea na matibabu japo mkono wake wa shoto bado umekufa ganzi na kichwa kinamuumauma.
amenituma nitoe asante sana kwa wote waliotuma na watotuma salamu za kumtakia apone haraka. anasema hana cha kuwalipa anamuachia jalali..

No comments: