Saturday, August 2, 2008

Kampuni ya Celtel sasa Kuitwa
Zain...
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Simu za Mkononi ya Zain(zamani Celtel)kwa Kanda ya Afrika Mashariki,Bashar Arafeh akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa jina hilo.
------
Kampuni ya simu za mikononi ya Celtel imebadilisha jina la biashara na kuanzia jana,inajulikana kama Zain.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Zain Kanda ya Afrika Mashariki,Bashar Arafeh alisema hatua hiyo pia inakwenda sambamba na kuunganishwa mabara mawili kwa mtandao mmoja.

“Kuibadilisha Celtel kuwa Zain ni mwanzo wa enzi mpya kwa wateja wa Celtel nchini Tanzania. Lengo ni kuwa kampuni ambayo inahudumia duniani kote,na baada ya mwaka 2011 kuwa miongoni mwa kampuni 10 bora duniani,”alisema.Arafeh alisema mabadiliko hayo haya athiri masuala ya hisa.Alisema serikali inaendelea kumiliki hisa asilimia 40 na asilimia 60 zitabaki kwa Zain.

Kwa mujibu wa Arafeh,kampuni hiyo ambayo ina miaka 10 tangu ianzishwe,imekuwa ikitoa huduma katika nchi 14 za Afrika na kwamba itaongeza huduma na kufikia nchi 15 mwisho wa mwaka huu.Habari na Anastazia Anyimike.Picha Mrock

No comments: