Fazul Abdullah Mohammed
Awatoroka Polisi...
Na Msimbe Lukwangule.
MTUHUMIWA wa ugaidi ambaye anadaiwa kuhusika na mashambulio ya mabomu katika ofisi za Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi,Kenya na Dar es Salaam Tanzania,Fazul Abdullah Mohammed(pichani)amefanikiwa kuwatoroka polisi waliokuwa wanakwenda kumkamata.Balozi hizo zilishambuliwa miaka kumi iliyopita.
Polisi wamesema kwamba wanaendelea kumsaka mtu huyo aliyewatoroka mwishoni mwa wiki.Fazul Abdullah Mohammed alifanikiwa kuwatoroka polisi katika Mji wa Malindi,ambako alikuwa anaishi na marafiki zake,BBC imeripoti.Mapema mwaka huu Mohammed,ambaye anatoka visiwa vya Comoro alipona chupuchupu wakati wa shambulio la Marekani nchini Somalia lililolenga kumwangamiza yeye.
Marekani imeahidi kutoa jumla ya dola za Marekani milioni 5 kwa mtu atakayewezesha kukamatwa kwake.Polisi wanawahoji watu waliowakuta katika nyumba hiyo.Zaidi ya watu 250 walikufa wakati wa shambulio la Nairobi ambalo inadaiwa Mohammed alishiriki kulipanga.
Mohammed inasadikiwa ndiye anayeongoza kundi la al-Qaeda kwa Afrika mashariki.
Mohammed inasadikiwa ndiye anayeongoza kundi la al-Qaeda kwa Afrika mashariki.

No comments:
Post a Comment