Saturday, April 12, 2008

SASA MVUA NOMA DAR

Mwenge wanakiona cha moto kutokana na ujenzi wa barabara ya sam nujoma.

Hapa ni njia ya kuingia sokoni Mwenge yaani kama mtu huna four-wheel ama magari ya wabarikiwa kama haya huingii labda ulipaki njiani ingawaje nayo kuna wakati yakiliingia shimo hilo vibaya nao hutaabika! Ila hapa wachina (wanatengeneza hiyo barabara) kwa nini walichimba na wakijua hiyo kazi wasingeweza kuifanya hadi hii leo maana tangu wachimbe ni miezi kama mitatu kama sikosei na zaidi imeshapita hilo dimbwi halikuwepo ila wachina wakachimba lami ambayo ilikuwa haina hata matatizo sijui sirikali inafanya nini maana ni mambo ya sirikali. Ila wachina na sirikali kuna nini hapo lakini ? au kuna harufu nyingine zaidi. Sasa wafanyabiashara wa mwenge wanalamika sana maana wanasema wateja wamepungua sana na kusababisha pato lao kushuka sana kutokana na hilo shimo na wao wanatoa malalamiko yao kupitia blog hii kuwa waangaliwe na wao au mpaka yatokee maafa zaidi ndio sirikali istuke kama kule mererani ? Sasa magonjwa ya mlipuko yakitokea hapo hamna atakae pona maana ni sehemu ambayo ni watu wengi wanaitumia kwa shughuli za kila siku.

Lakini kiboko ni kwa washabiki wa mpira awakitoka Uwanja wa taifa hii ni barabara ya lami Mandela road lakini shughuli ipo. Sijui kulikuwa na wachina wanachimba mji mzima ,eti mitaro ya maji machafu, sijui, sijui lakini nadhani iliziba!

No comments: