Thursday, April 17, 2008

Waziri Mkuu wa wanafunzi Mlimani (UDSM) Asimamishwa .......


WAZIRI Mkuu wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), Julius Mtatiro amesimamishwa masomo kwa madai ya kuhusika na fujo zilizotokea Februari 17 na 22 mwaka huu chuoni hapo.Ingawa katika orodha ya wanafunzi 18 iliyotangazwa juzi na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala wa kwanza kulia, kuwa wamesimamishwa masomo,jina lake halikuwamo lakini Mtatiro alisema kuwa alikabidhiwa barua jana ya kusimamishwa. Kwa mujibu wake aliambiwa kuwa amesimamishwa kwa sababu Kamati iliyoundwa na chuo kuchunguza vurugu hizo, imemtaja kuwa pia alihusika.Habari na Faraja Mgwabati

No comments: