Monday, April 21, 2008

Breaking News...*Andrew Chenge Ajiuzulu Uwaziri...



Aliyekua Waziri wa Miundombinu,Bw Andrew Chenge Pichani,amejiuzulu wadhifa huo hivi leo Kufuatia Kashfa Ya Akaunti yake ya nje ya nchi kukutwa na Mabililioni ya Fedha, Habari zaidi zinasema kujiuzulu kwa Waziri chenge kume kunapisha Tume inayochunguza shutuma hizo kufanya kazi zake kwa uhuru na Haki.
Kujiuzulu kwa Bw Chenge kunafatia Tuhuma dhidi yake za kujilimbikizia fedha, kuchapishwa na gazeti la The Guardian la Uingereza, ambalo lilieleza kuanza kwa uchunguzi dhidi ya waziri huyo baada ya wachunguzi kukuta ana zaidi ya dola za Marekani milioni moja (sh bilioni moja za Kitanzania)Kwa mujibu wa gazeti la Guardian,Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai nchini Uingereza ya Serious Fraud Office (SFO), inatarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo, ili kuangalia iwapo zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi za Uingereza milioni 28, ambazo ni sawa na Sh 70 bilioni, mwaka 2002.
Habari za Kujiuzulu kwa Waziri Chenge zimethibitishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw Salva Rweyemamu ambaye amesema,Rais Jakaya Kikwete amekwishaipokea barua ya kujiuzulu kwa Chenge na amemkubalia na akasema huo ndiyo uamuzi wa busara na ndiyo aliokuwa akiusubiria.Tutaendelea kuwaletea nyuzi zaidi Kadri tutakavyozipata..

No comments: