Tuesday, April 22, 2008
Wapinzani Watinga Tume ya Maadili..
Pichani ni viongozi wa vyama vya upinzani walipotekeleza ahadi yao ya kwenda kuuliza fedha na mali za viongozi wa nchi kwa kuwasilisha barua kwenye ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa umma wakitaka kukagua fomu za viongozi zinazotaja mali zao na vigogo na wabunge nchini akiwemo Rais Jakaya Kikwete jana jijini Dar es salaam.Hata hivyo juhudi za viongozi hao kupata fomu hizo ziligonga ukuta. akizungumza muda mfupi baada ya kushindikana kupata fomu zinazoeleza vigogo mbalimbali nchini wanamili mali kiasi gani,kiongozi mkuu wa cha cha TLP Bw Mrema alisema hadi sasa mawaziri wanne ambao wamejiuzulu wamefanya ushindi kufikia asilimia 40. alisema "Sasa hivi vita yetu ya ufisadi imefanikiwa kwa asilimia 40, mawaziri wanne ambao tuliwataja katika tuhuma za ufisadi wameshajiuzulu," alitamba Mrema.Picha na Msimbe Lukwangule.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Duh!!!! Hii imetulia wapinzani big up sana endeleeni namna hiyohiyo kwani ni njia mojawapo ya kulikomboa taifa letu linaloliwa na wachache!!!!!!
Post a Comment