Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza, SFO, ambayo ndiyo iliyofichua vijisenti vya aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Bwana Andrew Chenge, huenda ikawaliza vigogo wengine zaidi.
Chanzo cha gazeti hili kimedai kuwa, tayari taasisi hiyo imeanza uchunguzi wa kina dhidi ya vigogo kadhaa wa Tanzania.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, miongoni mwa vigogo wanaoliwa mingo na taasisi hiyo ni mawaziri kadhaa wa serikali ya awamu ya tatu iliyokuwa chini ya Bw. Benjamin Mkapa pamoja na wengine wa serikali ya sasa ya Rais Jakaya Kikwete.
Kwa hesabu za haraka haraka, chanzo hicho kimedai kwamba vigogo waliowekwa kwenye uchunguzi mkali hadi sasa wanafikia kumi ingawa majina yao hayakutajwa.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, uchunguzi huo wa SFO huenda ukawaliza vigogo kibao hasa wale wanaohusishwa na sakata la ununuzi wa rada kutoka kampuni ya BAE System ya Uingereza.
Wachunguzi hao wa Kitasha ndio waliobainisha kuwa Bw. Chenge ana mapesa kiasi hicho kwenye akaunti moja iliyo katika kisiwa cha Jersey.
Kadhalika ilieleza kuwa mapesa hayo yaliingia kipindi kile kile cha sakata za ununuzi wa rada iliyolalamikiwa sana na Watanzania kwa kile walichodai kuwa rushwa imetembea mno.
Sakata hilo lilipamba moto hadi Bw. Chenge akaachia ngazi mwenyewe. Hadi sasa nafasi yake iko wazi.
No comments:
Post a Comment