Thursday, April 24, 2008


Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiandamana leo mchana kuelekea ofisi za Utawala kulaani mauaji ya wenzao wawili waliouwawa kufuatia vurugu zilizotokea chuoni hapo jana.Picha na Christopher Lissa
----------
SERIKALI imetangaza kuwafutia udahili na kuwafukuza masomo wanafunzi waliofanya vurugu katika chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Taarifa ya serikali iliyosomwa bungeni jana jioni mjini hapa na Waziri wa Elimu na na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, ilieleza kwa kifupi kuwa wanafunzi hao wapatao 39 wa chuo hicho wamefutiwa udahili na hawataruhusiwa kujiunga na chuo chochote nchini.

“Waliofanya fujo leo (jana) wamefutiwa udahili na kufukuzwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na hawataruhusiwa kujiunga na chuo chochote,” alisema Profesa Maghembe katika taarifa hiyo bungeni saa 11.30 jioni leo.

Profesa Maghembe alisisitiza msimamo wa serikali kuwa haitawavumilia watu wanaofanya uhalifu na vurugu badala ya kusoma.

No comments: