Friday, April 25, 2008
Kitanzini: Hapa Walinyongewa Wazee Wetu
Kuna baadhi yenu mliotaka kujua zaidi ya kihistoria kuhusu Kitanzini, Iringa. Pichani Mzee Nzowa bado anakumbuka mahala hasa uliposimama mti uliotumika na Wajerumani kuwanyongea Wahehe. Mahala hapo palijulikana kama Kitanzini. Aliyefikishwa hapo alifungwa kitanzi shingoni na kuning'inizwa hadi kifo. Utotoni Mzee Nzowa alikua akiuona mti huo ingawa watu hawakuendelea kunyongwa hapo baada ya Mwingereza kuingia nchini. Mti huo wa kihistoria anadhani ulikatwa miaka ya 50 wakati wa kutengeneza barabara za mitaa. Hadi hii leo eneo hili linajulikana kama Kitanzini. Kwenye nchi za wenzetu wangeweka haraka mnara wa kumbukumbu ili kuitunza historia kwa vizazi vijavyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment