Saturday, April 26, 2008
Tabata Dampo Mambo Safiii...
Mmoja kati ya wakazi waliobomolewa nyumba zao katika eneo la Tabata Dampo Dar es Salaam, Aisha Msabaha akionyesha karatasi yenye namba yake ya nyumba wakati wa kuhakiki hati za nyumba hizo leo.Picha na Bernard Rwebangira
--------------
WAKAZI wa eneo la Tabata Dampo lililopo Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, jana kwa kushirikiana na maofisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, waliendesha zoezi maalumu la kutambua wamiliki halali wa nyumba zilizobomolewa na zinatarajiwa kulipwa.
Katika zoezi hilo lililochukua takribani siku nzima, wamiliki halali walipatiwa namba maalumu ya utambuzi wa nyumba zao na walipiga nazo picha.Mwenyekiti wa Mtaa wa eneo hilo, Julius Masanja alisema zoezi hilo linatokana na madai kuwa kuna watu wanaotaka kufanya utapeli kwa kujihusisha na malipo hayo.
Ofisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Daniel ole Mungai alisema watakaobainika kuwa ni wamiliki halali wataanza kulipwa kuanzia Jumatatu ijayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment