Saturday, April 26, 2008

Nyumba za Serikali Zilizouzwa Kinyume na Sheria Zarejeshwa...


Mbunge wa Vunjo (CCM) Aloyce Mrema, akiwasilisha hoja binafsi kuhusu uuzwaji nyumba
bungeni mjini Dodoma jana.

Mbunge wa Arusha Mjini (CCM) akichangia hoja binafsi ya uuzwaji nyumba za serikali
bungeni mjini Dodoma jana.

Mbunge wa Bukene (CCM) Teddy Kasela-Bantu akizungumza kuchangia hoja ya uuzwaji nyumba za serikali bungeni mjini Dodoma jana. Kulia ni Mbunge Mbunge wa Viti Maalum Chadema Lucy Owenya.
-------------
WIZARA ya Maendeleo ya Miundombinu, imekiri kuwapo na kasoro zilizojitokeza kwenye mchakato wa uuzaji wa nyumba za serikali na tayari watu wanne waliouziwa nyumba kinyume cha taratibu wamezirudisha na saba zisizostahili kuuzwa pia zimerudishwa.

Naibu Waziri, Dk. Milton Mahanga aliyasema hayo bungeni jana wakati akichangia hoja binafsi ya Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), aliyoiwasilisha akitaka kurejeshwa kwa nyumba hizo kwa sababu ziliuzwa kinyume cha taratibu.

Katika kuchangia hoja hiyo, Dk. Mahanga alikiri kuwa kweli zilijitokeza kasoro kwenye mchakato wa kuuza nyumba hizo na Tume iliundwa na inaendelea na kazi. Kwa mujibu wa Mahanga, kuna watu ambao hawakustahili kuuziwa nyumba lakini wakauziwa. Tayari nyumba nne zimerudishwa.

No comments: