Namshukuru Mungu kwa maishani yangu, zaidi sana namshukuru kwa kunipa nafasi ya kuendelea kupumua na kutoa mchango kwa nchi aliyoniweka ndani yake; Tanzania, nchi ninayojivunia pamoja na matatizo yote yanayojitokeza, ambayo yanakatisha tamaa.
Sekunde chache kabla sijaanza kuandika pasua jipu hii nimepokea taarifa ya kusikitisha ya kifo cha Ukiwaona Ditopile Ramadhani Mwinshehe Mzuzuri, ambaye leo hii nalazimika kuanza kutamka jina lake na neno marehemu! Mungu, ailaze roho yake mahali pema peponi.
Taarifa hizi zimebadilisha kabisa muelekeo wa makala niliyotaka kuandika, nimelazimika kumkumbusha Mhe. Edward Lowassa na Watanzania wenzangu japo ni kweli inasikitisha kusikia habari za kifo lakini kila mara tunaposikia habari hizi au kuona makaburi yatupasa kujifunza kwamba sisi sote tutapita katika safari hiyo na je, tufanye nini kabla siku hiyo haijafika? Kifo cha Ditopile na yaliyompata kabla ya kifo chake ni somo kubwa kwangu na viongozi tulionao madarakani na watakaofuata baadaye, somo lenyewe ni; Ili mtu yeyote afe na heshima ile ile aliyokuwa nayo, yampasa kuigharamia heshima hiyo.
Ndugu zangu, Watanzania wenzangu. Sitaki kuongea tena juu ya yaliyojitokeza kabla ya kifo cha Ditopile, sitaki kumhukumu, mwenye uwezo wa kufanya hivyo ni Mungu peke yake ambaye hivi sasa Ditopile yuko mbele yake kama ambavyo mimi nitasimama mbele yake siku moja, lakini jambo moja nataka kuliongelea kama njia ya kukumbushana ni juu ya viapo wanavyokula viongozi wetu na viapo wakiwa wameshika vitabu vitakatifu vya Mungu.
Huko nyuma nishaandika juu ya jambo hili, nikaonya kwa kusema Mungu hataniwi na si wa kufanyiwa mzaha hata kidogo kwani yeye ni Mungu na ana uwezo wa kuharibu! Leo tena nataka kukumbusha kwamba hili ni jambo la hatari sana kufanywa na mwanadamu mbele za Mungu na amesema mwenyewe katika maandiko yake kwamba atawaadhibu wote wanaofanya jambo hili.
Ditopile amekufa, ametanguha mbele za haki lakini pamoja na kifo chake, kiongozi huyu ataendelea kubaki mioyoni mwetu, atakumbukwa kwa yote aliyoyatenda mema na mabaya! Ndiyo maana ni jambo jema sana sisi wanadamu kuishi duniani na kutenda mema ili hata baada ya sisi kuondoka, matendo yetu yaendelee kutuwakilisha duniani! Ditopile amefanya mengi lakini litakalokumbukwa zaidi ni lile alilolifanya miezi michache kabla ya kifo chake, ambalo kwa hakika liliyafunika mema yote aliyoyafanya na kuonekana mtu asiyekuwa na maana, ndugu zangu hili ni somo kwetu tuliobaki hai, tunao uwezo wa kubadilisha mambo ambayo wanadamu wataongea kuhusu sisi baada ya kufa.
Katika hili la kubadilisha maneno yatakayosemwa juu yetu, sina budi kumshauri kaka yangu, ndugu yangu na Mtanzania mwenzangu, Edward Lowassa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania lakini akajiuzulu kwa sababu ya kashfa ya Richmond! Mtu huyu leo anaonekana fisadi, mwizi, mwenye tamaa ya utajiri na sifa nyingine nyingi chafu! Lowassa anafahamu wazi kwamba, ikitokea akapumzika kama alivyopumzika ndugu yetu Ditopile, sifa atakayoiacha duniani ni "alikuwa fisadi, alikuwa mwizi mpaka akajiuzulu" Hii ni aibu kubwa, si kwake tu bali familia na ukoo wake!
Ni ukweli ulio wazi kwamba hata wajukuu zake watakaokuja baadaye na kujitambulisha kwa jina la Lowassa, watahusishwa na Richmond, wanaweza kuhusishwa na wizi na ufisadi, laana hii ikaendelea kuwaandama maana siyo rahisi kuifuta katika historia! Rafiki yangu mmoja alilazimika kujitambulisha kwa jina la Maumba alipotatowa kufanya hivyo kwa sababu tu kuna mtu mmoja jijini Dar es Salaam ambaye pia aliitwa Maumba akaingia katika kashfa ya kubaka watoto wa shule ya msingi! Kila rafitoyangualiposema"...naitwa Maumba" watu walimuuliza "yule Maumba wa ..." akaamua kuachana na jina la Maumba na kuchagua jina jingine la ukoo.
Huu ni ukweli, kuna wakati mwingine tunaadhibiwa kwa makosa yaliyofanywa na waliotutangulia, tunakufa kwa sababu Adam na Hawa walikula tunda bustanini! Jina la Lowassa limechafuka na anayo kazi kubwa ya kufanya kulisafisha na inawezekana kubadilisha kesho kwa tunayoyafanya leo, lazima Mhe. Lowassa afanye kazi ya ziada kubadilisha picha hii ambayo Watanzania wanayo vichwani mwao kuhusu yeye na wataendelea kuipandikiza vichwani mwa vizazi vijavyo.
Hebu nitoe mfano wa Afred Nobel, mwanasayansi aliyejipatia utajiri mkubwa kwa kutengeneza mabomu yaliyoua mamilioni ya watu dunia nzima, siku moja ndugu yake alikufa na watu wakafikiri aliyekufa ni yeye Afred Nobel, mengi yakaongewa na kuandikwa katika vyombo yya habari akabahatika kuyasoma na kuyasitoa.
"Aliyejitajirisha kwa kuua watu hatimae naye amekufa!"
Hivi ndivyo dunia ilivyozungumza, jambo hili likamuumiza Afred Nobel baada ya kufahamu totakachozungumzwa juu yake atakapokufa! Moyoni mwake akasema "Nitaibadilisha historia, hakuna atakayesema hivyo nitakapokufa!" Kazi ya Afred Nobel kuanzia siku aliyotamka maneno hayo ikawa ni kutafuta jambo atakalolifanya ili akifa watu waseme kitu tofauti kuhusu yeye, hili ndilo jambo ambalo Mhe. Edward Lowassa anatakiwa kulifanya pia.
Badala ya kuendelea kugombana, mwaka 1895, Afred Nobel
alianzisha tuzo ya Nobel (Nobel prize) aliypitoa kwa watu mbalimbali duniani kama njia ya kuwaheshimu kwa mchango walioutoa katika kuiendeleza dunia na wanadamu wenzao na baadaye alipokufa watu hawakumwongelea kama mtu aliyetengeneza mamilioni ya fedha kwa kuwaua binadamu wenzake, bali walimtaja kama mwanzilishi wa tuzo ya Nobel! Akawa amefanitowa kubadih historia yake.
Leo hii itowa imepita miaka 113 tangu Afred Nobel aanzishe tuzo ya Nobel, anaendelea kuheshimiwa na watu maarufu duniani kama Profesa Wangari Maathai wanaendelea kupokea tuzo yake.
Hili ndilo jambo ambalo Edward Lowassa anatatowa kulifanya badala ya kuendelea kugombana na watu anaoona kama wamemchafua, amuige Afred Nobel kwa kufanya mema katika jamii, walasikuhangaika katika magazeti kujisafisha. Mema yake muda si mrefu yatafunika uovu wote anaodaiwa kuufanya na atakapopumzika kama ilivyotokea kwa Ditopile watu watamkumbuka kwa mema hayo, ndiyo, hawataisahau Richmond lakini hawatakuwa na hasira sana kama ambavyo leo hii sina hasira dhidi ya Afred Nobel ingawa ni kweli mabomu bado yanaendelea kuua watu. Lowassa akimwiga Nobel atakuwa ameiepushia familia na ukoo wake aibu. Hayo ni mawazo yangu, mtu anaruhusiwa kuyapuuza.
Si Lowassa tu anayetakiwa kufanya hivi, wapo watu wengi, hivi karibuni nimesikia habari za Chenge, kama yanayosemwa juu yake ni ya kweli basi pia anatakiwa kuchukua hatua za Afred Nobel, Digrii ya Harvards peke yake haitamsaidia sana bali abadili mwelekeo na kuwa muadilifu ili ajiepushe na aibu itakayompata mwisho wa safari yake! Huu kwangu ni ukweli.
Nchi hii imejaa viongozi wengi wachafu, waovu na waliojaa hofu sababu ya maovu yao na wanafikiri wana uwezo wa kuficha uovu huo mpaka mwisho wa safari! Niwahakikishie, hakuna mtu hata mmoja mwenye uwezo wa kufanya hivyo, siku itafika uovu utajianika wenyewe na aibu itakayopatikana itawafanya viongozi hawa kumaliza maisha yao vibaya!
Jambo kubwa wanalotakiwa kufanya viongozi wetu wa leo ili kuepusha aibu na kumaliza maisha yao vibaya ni kuwa waadilifu wa kweli, wawazi na wenye kutii viapo walivyokula! Si kuingia madarakani, kuapa na kuenenda kinyume na viapo ili kujipatia utajiri kwa njia ya mkato ambayo mara nyingi huishia pabaya.
Ndugu zangu, Watanzania wenzangu, acha niishie hapa kwa leo nawatakieni wiki njema yenye mafanikio na tukutane wiki ijayo katika ukurasa huu huu, Kwa Mhe. Lowassa ninasema hata kama leo hii anaonekana mwizi, fisadi bado anayo nafasi ya kubadili histori yake kama alivyofanya Afred Nobel kwa kufanya mema katika jamii, hii itasaidia kufunika uovu kwa wema jambo linaloweza kumwinua mpaka juu kwa mara nyingine tena kama ndoto zake zilivyo.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
Muhandishi ni Erick J. Shigongo.
No comments:
Post a Comment