Thursday, June 24, 2010

Traffic
Askari wa barabarani bwana !!

Hawa bwana wako safi sana utapenda wanapofanya kazi zao. Kweli wanahitaji pongezi kwa kazi wanazo fanya kila siku . Natumai wadau wote mnakubaliana nami kuwa hawa jamaa kweli wanapiga kazi si kitoto .
Kero yao bwana kubwa niubabe mfano wanapokukamata . Kama huwajui utasema kweli leo ndio mwisho wa dunia. Wanakuwa wanatisha hao na mambo mengi ili kutengeneza mazingira ya rushwa na hao sio wote tuwe makini hapo. Maana wanasema samaki mmoja akioza ni wote hao waenga ila mie nasema akioza mmoja sio wote. Ila wanatia dowa wenzao kwa hiyo kwa maoni yangu wajirekebishe katika hilo.
Ila lingine linalonibowa kwa hawa wajomba zangu na maanti zangu ni kuwa makini na pale wanapo simamisha magari kwa kusimama mbele ya magari.
Sijui huwa hawakumbuki kuwa haya magari kuna wakati yanashindwa kushika break na hapo wanahatarisha maisha yao kwa uzembe wao wenyewe. mimi naomba mbadilike katika hili kwa maana bado tunawahitaji sana katika ujenzi wa taifa letu ambalo linaitaji nguvu kazi pasipo kuzipoteza.
Hayo yangu ya leo tu .

No comments: