Monday, June 28, 2010

Mwenyekiti wa kamati ya Redds Miss Kinondoni Bw. Boy George wa pili kutoka kulia akiongea mbele ya waandishi wa habari leo kwenye mgahawa wa Hadees wakati alipotangaza zawadi kwa washindi watakaopatikana katika shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Boy George amesema mshindi wa kwanza katika shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 1,500,000 zitakazotolea na wadhamini ambao ni Giraffe Ocean View Hotel wakati mshindi wa pili atapata shilingi milioni 1,000,000 zitakazotolewa na Tanga Beach Resort, mshindi wa tatu atapata shilingi laki 800,000 mshindi wa nne na wa tano watapata kiasi cha shilingi laki 300,000 kila mmoja na washiriki wengine kila mmoja atapata kifuta jasho cha shilingi 150,000.
Taji jipya la mrembo mwenye akili, kujiamini na uwezo wa kujieleza yaani Miss Rolls and Skills litatolewa na Jarida la Namba 10 na mshindi atapewa shilingi laki 500,000 na mshindi wa taji la kipaji atajipatia shilingi 200,000 wakati mrembo mwenye nidhamu atapata shilingi elfu 50,000.
Burudani itatolewa na Bendi ya THT na Sebene la nguvu kutoka bendi ya African Stars wana wa kutwanga na kupepeta, huku kiingilio katika shindano hilo kikiwa shilingi elfu 50,000 kwa VIP na shilingi 20,000 kwa viti vya kawaida.
Katika picha kulia ni Selemani Mbuguni mratibu habari wa shindano hilo na Rahma George mkurugenzi wa Miss Kinondoni wa tatu kutoka kulia pamoja na mwalimu wa warembo Lulu Ibrahim ambaye ndiye Miss Kinondoni 2009 pamoja na warembo wanaoshiriki shindano hilo.
Kwa msaada mkubwa wa blog ya John.

No comments: