Saturday, June 26, 2010

Mr Sugu, Mkoloni na G. Solo wajiunga CHADEMA
Wasanii maarufu wa muziki nchini Tanzania Joseph Mbilinyi aka Sugu lias Mr II, Fred Malick aka Mkoloni na Gerald Mwanjoka aka G. Solo wamejiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kukabidhiwa kadi zao za uanachama. Tukio hilo limechukua nafasi katika Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA, zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Pichani ni wanamuziki hao na Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mnyika.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Joseph Mbilinyi Mr Sugu akipokea katiba ya CHADEMA, kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, baada ya kujiunga rasmi na chama hicho jana katika Makao Makuu ya CHADEMA, Kinondoni, jijini Dar. Chanzo, habari Zaidi na picha:
BOFYA HAPA

No comments: