Saturday, September 26, 2009

ujumbe mahususi wa wiki ya usalama barabarani 2009

Je, umesimamishwa na polisi wakati ukiendesha gari, pikipiki au baiskeli?

zijue haki na wajibu wako !

Bila kufuata sheria na kanuni za usalama
barabarani kutakuwa na vurugu katikabarabara zetu.

Soma na ujifunze kanuni, Sheria Mpya za Barabara – iwapo kila mmojaatazifuata sote tutafika tunapokwenda kwa urahisi na usalama zaidi. Polisi wana kazi ngumu na muhimu sana ya kutekeleza sheria. Lazima kushirikiana nao,isipokuwa kama wanatenda kinyume na sheria.


Maelezo hayo ni muhtasari wa mwongozo wa nini ofisa wa polisi aliyevaa sare anaweza kufanya kisheria na kukueleza ni wakati ganianakusimamisha uwapo barabarani.


Unaweza ukapenda kukata maelezo haya na kuyaweka kwenye gari lako – lakini kumbukakwamba ni mwongozo tu.


Mamlaka ya kusimamisha gari lako:

Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha gari lako – kamaatakupa ishara ya kusimama, punguza mwendo kwa usalama na utoke barabarani – piaanaweza kukuuliza jina na anwani yako na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya Usalama Barabarani (RTA),s.78).


Leseni ya kuendesha gari:

Ofisa wa polisi anaweza kuomba kuona leseni yako yakuendesha gari – anaweza kukataa fotokopi – hata hivyo, unaweza kuamua kupelekaleseni yako ndani ya siku tatu kwenye kituo cha polisi kilichochaguliwa na ofisa.Ili kuepukamatatizo, wakati wote tembea na leseni yako kwenye gari (RTA s.77).

Hati ya usajili:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua maelezo ya usajili kama yanavyoonyeshwa kwenye kibandiko cha usajili – gari lazima liendane na maelezo yakwenye kibandiko, lakini vitu vidogokama rangi iliyofifia au iliyobanduka haijalishi (RTA s.13).

Leseni ya barabarani, na bima ya gari:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama umebandika leseni halali ya barabarani nakibandiko cha bima kwenye kiwambo cha upepo cha gari lako (kioo cha mbele).

Kunyang’anywa:
Ofisa wa polisi HANA haki ya kuondoa vibandiko na kuchukua leseni
isipokuwa kwa mujibu wa sheria.

Mikanda ya kiti ya usalama:
Wewe na abiria wako wa kiti cha mbele ni lazima mfunge mikanda ya kiti ya usalama unapoendesha (gari iwe inatembea au imesimama) – unatendakosa kama unaendesha wakati abiria wako hajafunga mkanda wa kiti wa usalama (RTAs.39.11). Hata hivyo inashauriwa abiria wote wafunge mikanda.

Kuendesha baada ya kunywa pombe:
Kama ofisa wa polisi anakuhisi umekunywa pombe na huwezi kulidhibiti gari ipasavyo,anaweza kukutaka upimwe (kipimo cha kupumua au kipimo cha damu) kuona kama kiasi chapombekwenye damu yako ni zaidi ya kiwango kilichoelezwa. Kama ukikataa utakuwa na hatiaya kosa (RTA s.44, s.45, s.46).

Kutumia simu ya mkononi wakatiunaendesha:
ingawa sheria haikatazi hili mahususi, ofisa wa polisi anaweza kuona kuwa unatenda kosa la “kuendesha kwa uzembe” (RTA, s.42, s. 50).

Mwendo kasi:
Unapaswa kuzingatia kikomo cha mwendo kasi, (ikiwa ni pamoja na km 50kwa saa katika maeneo ya hatari, ambayo yanaweza yasiwe na alama) – ofisa wa polisianaweza kupima mwendo kasi wako kwa namna mbalimbali - hata hivyo, unawezakupinga ushahidi wake mahakamani (RTA s.51, s.73(2)).

Kustahili kuwepo barabarani:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama gari lako liko katika hali ya usalama kiufundi. Matairi, breki, taa, indiketa na usukani lazima viwe vinafanya kazi vizuri –unawezakutakiwa kupeleka gari mahali litakapokaguliwa kikamilifu na mkaguzi wa magari wapolisi (RTA, s.39.1, s.81).Unashauriwa kupeleka gari lako kukaguliwa na polisi kila mwaka. Pata stika ya usalama barabarani, cheti cha ubora wa gari, au barua kutoka polisi kama ushahidi kwamba gari lako limekaguliwa.

KAMA OFISA WA POLISI ANAKUTUHUMU KWAMBA UMEFANYA KOSA:
Mara nyingi utapewa uchaguzi wa kukubali kosa na kulipa faini ya sh. 20,000 kwaofisa wa polisi, au kwenda mahakaman ili kujibu mashtaka. Ofisa ataandika maelezokwenye Fomu ya Polisi ya PF 101, na nyote wawili mtatia saini – kamwe usilipe faini bila ya kupata nakala ya Fomu iliyotiwa saini. Unaweza kwenda na ofisa kwenye kituo cha Polisi kutoa maelezo. Kama unakubali kosa, lakini huwezi kulipa faini, ofisa wa polisi atakueleza jinsi ya kutuma malipo kwa kamanda wake wa eneo (RTA, s.95).

KAMA UNAFIKIRI OFISA WA POLISI AMETENDA KINYUME CHA SHERIA AU AMEKOSEA KWA NJIAYOYOTE UNAWEZA KUTOA MALALAMIKO: muulize ofisa jina lake, cheo na namba, na anwani ya kituo cha polisianakofanyia kazi (unayo haki ya kuuliza hilo.) Kisha peleka malalamiko ya maandishikwa Ofisa Msimamizi Mkuu – ambaye atachunguza na kujibu.

Tusaidie kuwafanya maofisa polisi wetu kuwa waaminifu –
usitoe rushwa na usipokeerushwa.
Said A. Mwema
Inspekta Jenerali wa Polisi

No comments: