taswira za mji mkuu wa uswazi
Kaka Kadidi,
Basi bwana blog leo jioni nilikuwa kwenye viunga vya mji wa Mbabane ambao ni makao makuu ya nchi ya Swaziland. Yaani Ofisi zote za Serikali zipo hapa pamoja na maduka makubwa ya nguo na vyakula yapo katika eneo hili.
Eneo lipo juu zaidi toka usawa wa bahari, ni la milimani ukilinganisha na kitogoji cha Lobambo eneo la Ludzidzin ambako Reed Dance hufanyikaga katika Palace (jumba la mfalme) la Mama yake King Msawti III.
Mji wa Mbapane upo juu kama unatokea eneo la Ezulwini, yaliyopo makazi ya King Mswati, na hali ya hewa yake huwa ya baridi sana, kwa haraka haraka unaweza kufananisha na eneo la Mbeya kwa wale waliofika Mbeya wanaweza kupata picha kamili.
Aidha, nchi hii ina wakaazi wanaokadiriwa kufikia milioni 1.2 na eneo lake kama moja za wilaya hapo Bongo! picha hizi zinawasilisha taswira ya mji wa Mbabane, na hapa ni city centre yao, hakuna tena kama hapa.
Naomba kuwasilisha...
Mdau wa muda wa Swaziland
No comments:
Post a Comment