Wednesday, September 9, 2009

libeneke la yale yaleeeee ya barabarani .....
Habari kaka Kadidi,

Sijui utanisaidia vipi kuiweka hii na ningeshukuru kama ingefika kwa wahusika. Maeneo ya Veta nilikuwa naelekea nikiwa na gari aina ya Surf. Ni kweli kioo chake cha mbele kina crack na hayo matatizo mengine madogo madogo lakini gari iko kwenye good condition.

Askari alitukamata na akawa anatengeneza mazingira ya rushwa. Kwa kweli nilimsisitiza sana aandike notification na pia namba yake ya kazi. Aliponipa karatasi nikamhoji

- mbona hii ni note paper na siyo notification ya polisi yenye number na kila kitu.

- kwa nini unaniambia niache gari nikalipie Changombe polisi ndiyo nirudi kuchukua gari.

- Notification haina namba ya gari wala mhuri wala signature.

Baada ya kubishana kwa muda mrefu na kwa kuwa nilidhamiria kuona mwisho wa hii nilihakikisha nabaki na hii 'notification' (pichani) na aling'ang'ania nimpe Tsh 10,000 ambayo nilimpa ili nipate nafasi ya kuonyesha hali halisi ya hawa polisi wetu.

Tafadhali usitaje jina wala e mail yangu. Ila kama ni wahusika watataka kuwasiliana na mimi niko tayari . Kama ameandika namba ya uongo basi nitatoa picha yake niliyompiga.

No comments: