kanumba arejea bongo baada ya masaa 24 sauzi

Mapema leo, Afisa Uhusiano wa Multi Choice Tanzania Bi. Furaha Samalu, aliiambia Globu hii kuwa Kanumba na mastaa wenzie walialikwa kwa muda huo wa saa 24 ndani ya jumba hilo kwa nia ya kuzindua shindano lenyewe. Alisema Kanumba keshamaliza muda wa kuwa huko jana na huenda akarejea leo. Duru za karibu na Kanumba zimethibitisha kwamba keshatua na yuko kwao Temeke anapumzika baada ya kazi ya masaa 24....
Kuwamo kwa Kanumba kwenye jumba la Big Brother kulileta msisimko wa aina yake, hasa kwa wabongo wa ndani na nje ya nchi, wengi wakisema haya na yale kuhusu mbinu za mawasiliano alizokuwa akitumia SupaStaa huyu. Wengi wamemsifu kwa kuweza kuonesha kipaji cha ku-act kama hamnazo wakati yuko fiti ile mbaya, ikizingatiwa kwamba yeye ndiye staa pekee wa filamu aliyepata mwaliko Hollywood na pia London ambako ameshuti filamu za kimataifa itayotoka muda si mrefu ujao.
Bongo tuna historia njema katika Big Brother, ambapo awali mdau Mwisho Mwampamba aliwahi kushika nafasi ya pili katika shindano la ukweli la Big Brother kasha Richard akifanikiwa kuibuka kidedea katika Big Brother Africa na kulamba dola 200,000. Safari hii inasemekana mwakilishi wetu ni mwanadada, lakini jina limehifadhiwa.
Redio mbao zimekuwa zikimtaja Wema Sepetu na mwingine anayejulikana kama Ghandi. Jumapili hii wasichana washiriki wataingia mjengoni na ndipo mwakilishi wetu atajulikana.
No comments:
Post a Comment