Tuesday, September 29, 2009

neshno jipya: yale yaleeeeee......

Habari za kazi kadidi
kama anavyojiita mwenyewe,

Uwanja wetu mpya wa taifa ulishakamilika muda mrefu na kufnguliwa lakini kama taswira inavyoonekana yale mabati yanawekwa na kuzungushiwa kama uzio wakati wa ujenzi mpaka leo hayajaondolewa yapo yapo tu kama yanavyoonekana yanaleta picha mbaya na kuharibu taswira ya uwanja hapo

Mdau mwanaharakati
awadhi juma issa offered trial with academia sporting in portugal

Academia Sporting Africa of Lisbon, Spain, has offered an opportunity to Awadhi Juma Issa from the Tanzania Soccer Academy a five-day trial period at Academia Sporting Portugal. Academia Sporting Africa hopes that Awadhi will take the opportunity to show his ability and showcase the African flair.

Mdau Israel Saira
London.
Ni nani katika hawa warembo atavaa taji la Redds Miss Photogenic 2009?
namba 00027
namba 00000
namba 0001
namba 0002
namba 0003
namba 0004
namba 0004
namba 0005
namba 0006
namba 0007
namba 0008
namba 0008
namba 0009
namba 00010
namba 00011
namba 00013
namba 00014
namba 00015
namba 00016
namba 00017
namba 00018
namba 00019
namba 00020
namba 00021
namba 00022 namba 00023
namba 00024
namba 00025
namba 00026
warembo 29 wa Vodacom Miss TZ 2009 wanaochuana kuwania taji la Redds Miss Photogenic 2009, katika shindano linaloratibiwa na globu ya jamii ya issamichuzi.blogspot.com na kudhamniwa na kilaji cha Redds Premium Lager.
Mshindi atapata shs. 1,000,000/- taslimu, mkataba wa mwaka mmoja kufanya kazi za umodo na kampuni inayongoza ya umodo nchini ya Beautifl Tanzanie Agency pamoja na portfolio ya ulimbwende. Mdau unaombwa kupendekeza ni nani kati yao ni photogenic ama mrembo mwenye mvuto wa picha.
Mshindi atatangwazwa October 2, 2009 siku ya fainali za Vodacom Miss Tz 2009 zitazofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Conference Centre jijini Dar. Kazi kwako mdau......


Utafiti unaonyesha kuwa kusikiliza MP3 kwa sauti kubwa kwa saa moja kwa siku, kunaweza kuleta madhara makubwa katika kusikiliza kwa mtu. Kwa mujibu wa utafiti huo, kusikiliza mziki kwa sauti kubwa yawezekana kukapelekea mtu kusikia sauti za ajabu ajabu masikioni.
Uchunguzi uliofanywa na taasisi moja ya wasiosikia umeonyesha kwamba, watu wenye umri wa miaka 16 mpaka 34, husikiliza muziki kwa sauti kubwa bila kujali madhara yake . Wataalamu wanasemakwamba, kusikia sauti kama ya mruzi masikioni, au sauti nyinginezo ni kwa sababu ya kusikiliza mziki kwa sauti kubwa, ambako husababishwa na kuharibika seli za masikio kutokana na sauti kubwa ya mziki na kwa muda mrefu.
Uchunguzi uliofanywa barani Ulaya umeonyesha kwamba, kati ya watu 10 wanaotumia mp3, mmoja kati yao anakabiliwa na matatizo ya kusikia.
Hivo basi wataalamu wanatushauri kutosikiliza mziki kwa sauti kubwa, hasa wakati wa kufanya mazoezi kwa kutumia vifaa vya mazoezi au wakati wa kukimbia, kwani watu wengi kufikiria kuwa kila wanapongeza sauti ya mziki wakati wa mazoezi ndivyo wanavyoweza kuwa na mbio zaidi, suala ambalo si kweli.
JK afungua jengo la ubalozi wetu Washington DC
JK akifunua kitambaa kufungua rasmi jengo jipya la ubalozi jijini Washington Marekani
Jengo jipya la ubalozi jijini Washington Marekani ambalo JK alilifungua. Jengo hili limenunuliwa na serikali ya Tanzania kwa jumla ya dola za kimarekani $10,415,000. Chini JK akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Balozi iliyopo katika jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania jijini Washington Marekani .Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na wapili kushoto ni Balozi wa Tanzania Washington Ombeni Sefue

JK akisalimiana na wageni mbalimbali na mabalozi waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa jengo jipya la ubalozi jijini Washington Marekani zilizofanyika
JK akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la ubalozi jijinji Washington Marekani. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu





Saturday, September 26, 2009



HEBU CHECK DEREVA TAXI HUYU WA TEMEKE.
mzee yusuf alipeleka jahazi awamu mpya
katika kuonesha umahiri na ubunifu wa hali ya juu ulioipeleka jahazi modern taarab katika bahari kuu ya muziki huo nchini, mzee yusuf na kundi lake sasa wana madansa katika maonesho yao ambao linapopigwa sebene hufanya vitu si vya kawaida jukwaani. hii ilikuwa usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa bwawa la kuogelea wa city garden hotel gerezani (zamani railway club) dar
mzee yusuf akiongoza jahazi wakati wa shoo hiyo kali
mbunge wa temeke mh. abbas mtemvu alishindwa kujizuia na kuja kumtuza mzee yusuf kwa vitu vyake vya uhakika.
baadhi ya malkia wa jahazi
mpiga kinanda anayepagawisha
mkono wa dhahabu akipeleka wadau dubai huku shoto akionekana thabiti mtoto wa ilala akipapasa kinanda. listi imetimia jahazi modern taarab



ubunifu

Sanamu ya mkono ambao unazunguka kwa nguvu ya kupulizwa na upepo.Ubunifu wa aina hii katika sehemu za maji unapendeza sana.
Mdau K.Mmbando
TBL yaipiga jeki kamati ya usalama barabarani
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu akibandika stika kwenye gari Dar yenye maneno yanayotahadharisha madereva kutoendesha magari huku wakiwa wamelewa. Stika hiyo ni moja kati ya 4000 zilzotolewa msaada na TBL kwa Kamati ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Jana. Pia TBL ilitoa msaada wa fulana 800 kwa kamati hiyo. Wa pili kushoto ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, James Kombe,
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu (kushoto) akimkabidhi moja kati ya fulana 800, Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, James Kombe, ikiwa ni msaada kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama itakayoadhimishwa mkoani Mbeya kuanzia Septemba 28 hadi Oktoba 3, Mwaka huu. Katika hafla hiyo iliyofanyika Dar jana, TBL walikabidhi pia msaada wa stika 4000, vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 10.


dereva anaposusa kuendesha gari lililoshona

Kaka Kadidi2!
Basi bwana siku ya Idd ili kuwa taabu kidogo ya usafari hapa London. Nilipanda bus hili maeneo ya East Ham kuelekea Walthamstow, na tulivyofika mitaa green street abiria kibao wakapanda. Dereva akanuna na kususa kuendesha Bus eti sababu ya health and safety risk. Ebo fikiria hapo ingekuwa Kibongo- bongo ingelikuwaje. Ajabu na kweli ni kwamba hadi naondoka abiria ambao wengi wao walikuwa ni wa asili ya Asia walikataa katakata kuteremka. Sijui kwa bongo mambi yangekuwaje hapo??

Mdau Diaspora writer
migo migo enzi za mwalimu

sehemu ya magomeni mapipa jijini dar enzi za mwalimu
Kibaka wa Blackberry anaswa mayfair plaza leo
Kaka mambo vipi, mrushe huyu jamaa amekamatwa akiiba simu aina ya BlackBerry 8310 katika duka la moja Mayfair Plaza jijini Dar mchana huu. Kasema anaitwa Joseph Mbuya Mkazi wa Mikocheni A. Hapa akiwa chini ya ulizi mkali kuepusha wadau wenye hasira kali wasimfanyizie…!
Mdau DH