Tuesday, February 23, 2010

tutazzzzzz
Habari za leo Mdau,
NAOMBA NIWEKEE KWA WADAU
Nimatarajio yangu wote ni wazima na mnaendelea vizuri na kazi. Kwa kipindi cha miezi kadhaa sasa nimejaribu kufuatilia adha kubwa tunayoipata sisi Wakazi wa Temboni, Kwa Msuguri, Mbezi, Kibamba na kuendelea along Morogoro Road.
Kero hii kubwa hasa nyakati za asubuhi (saa 11 alfajiri na saa 2 asubuhi) na jioni (kuanzia saa 10 hadi saa 3 usiku) huwa inasababishwa na TUTA (BUMP) lililowekwa na TANRORADS eneo la Kimara Stop-Over.
Yes, I agree with Kinondoni Municipal Council na wadau wengine idea ya kuwa na hili tuta ni kupunguza mwendo kasi wa Mabasi, Malori, Daladala,Taxi Drivers n.k. Lakini ukifuatilia kwa karibu zaidi utaona hakuna tija yoyote inayopatikana na uwepo wa hili tuta pasi na kusabibisha unnecessary traffic congestion.
Wadau hii kero inaongezeka day by day na ni hakika siku moja it will reach its climax na kusababisha usumbufu mkubwa kwa Wananchi. Nafikiri ni vyema sasa Wadau tukajipanga na kwenda kumwona Manager wa TANROADS - DSM na kukaa naye meza moja ilikuweza kutatua kero hii kubwa.
I know kila mtu anayetumia barabara hii anaguswa na kero hii na huwa tunazungumza zungumza tu mitaani bila ya kufuatilia kwenye ngazi husika. Nafikiri ni sasa ni muda muafaka tukahamasishana na kwenda TANROADS ili kuweza kupata ufumbuzi. Ndugu mdau, the above is my opinion naomba opinion yako ili tuweze kujua way forward.
Regards, Mdau Albert

No comments: