Monday, February 22, 2010

simba, we acha tu; yairarua moro united 4-1 Jana
kocha wa simba Patrick Phiri akiwapongeza vijana wake kwa kuichapa Moro United bao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uwanja wa Uhuru jijini Dar jioni jana.
Golikipa wa Moro United, Mohamed Abdallah akiusindikiza kwa macho mpira uliopigwa na Emmanuel Okwi ukijaa wavuni na kuhesabu bao la kwanza kwa Simba jana.
Mshambuliaji harai wa Simba Ulimboka Mwakingwe, (kulia) akimtoka beki wa Moro United, Stephano Mwasika wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika jana jioni kwenye Uwanja wa Uhuru ijini Dar. Simba ilishinda 4-1.
Beki wa Simba Juma jabu akimtoka mchezaji wa Moro United, Yona Ndabila, na kuifungia timu yake bao la 4 wakati wa mchezo wa Ligi ya Vodacom uliofanyika jioni jana Uwanja wa Uhuru jijini Dar . Picha zote na Francis Dande wa Globu ya Jamii



No comments: