IGP Saidi mwema aibuka kutegua kitendawili cha pingu
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchni, IGP Said Mwema, akiongea na wanahabari mchana huu ofisini kwake jijini Dar. Shoto ni Afande Abdulrahman Kaniki.
IGP Mwema amesema kuwa suala la Jerry Muro kumiliki pingu linachunguzwa na Jeshi la Polisi na tayari timu ya uchunguzi imeshaundwa ili kubaini uhalali wa umiliki wake ili kuondoa utata uliojitokeza kuhusu raia kumiliki pingu.
IGP Mwema hakusema kama ni kosa ama la kumiliki pingu ila ameahidi kutegua kitendawili hicho baada ya uchunguzi huo.
IGP Mwema amesema ameunda kikosi cha askari polisi na kuwaagiza kusoma sheria na kuitafsiri vema ili kubaini ukweli wake katika umiliki wa pingu kwa raia.
"Si vibaya kukiri ujinga katika jambo usilolifahamu ndio maana nimeagiza vijana wangu kulifanyia uchunguzi suala hili kwa kupitia vifungu vya sheria na kutoa tafsiri yake kuhusu umiliki wa pingu kwa raia.
"Si vibaya kukiri ujinga katika jambo usilolifahamu ndio maana nimeagiza vijana wangu kulifanyia uchunguzi suala hili kwa kupitia vifungu vya sheria na kutoa tafsiri yake kuhusu umiliki wa pingu kwa raia.
"Baada ya siku mbili nitawaita tena ili kuwapa ufafanuzi wa kina juu ya pingu hizi za Jerry Muro na pingu nyingine. Tutajua sheria inaeleza nini ili jamii ifahamu suala hilo na kuondoa utata uluiojitokeza kuhusiana na raia kumiliki kifaa hicho kinachotumiwa na majeshi kudhibiti uhalifu", alisema na kuacha wanahabari wakifurahi kwa uwezo wake wa kujieleza pasina kutumia jazba wala vitisho.
IGP Mwema ameongea na wanahabari chache baada ya watuhumiwa watatu ambao ni Mtangazaji wa Kituo cha luninga cha TBC1 Jerry Muro, Edmund Kapama na Deogratius Mugassa, kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kujibu tuhuma za kula njama, kushawishi kupokea rushwa.
No comments:
Post a Comment