Monday, February 8, 2010

matokeo ya fom foo yamliza mdau
Nimepokea kwa huzuni sana matokeo ya kidato cha nne kwa watahiniwa waliofanya Mtihani mwaka 2009.
Licha ya kuwa ufaulu umeshuka kwa asilimia 11.2 ila ukiangalia kwa makini takwimu hizo ni za kuhuzunisha na nimeshidwa kujua ni nani hasa wa kupewa lawama au kuwajibika kutokana na haya matokeo maana ni aibu kwa nchi yetu ya Tanzania.

Watahiniwa 339,925 walifanya
mtihani huo na matokeo ni kama ifuatavyo:
Ukiangalia takwimu hizo unaona katika kila watahiniwa 100 watahiniwa 17 ndiyo wenye angalau daraja la kwanza hadi la tatu ambao kwa uzoefu ndiyo wenye nafasi ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano na cha sita.

Watahiniwa 82 katika kila watahiniwa 100 wamepata daraja na nne na sifuri. Mbaya zaidi ni kuwa zaidi wa watahiniwa 65,708 ndiyo wamepata daraja la sifuri yaani hao ni kwa mwaka mmoja tu. Tanzania tumetengeneza watanzania 65,708 wenye sifuri hii inasikitisha sana yani hawa wote hawata pata vyeti na elimu yao ya kidato cha nne na jinsi elimu yetu ilivyo hao wote hawana ujuzi wowote labda kusema wataenda wakajiajiri sehemu hiyo ni hakuna.

Watanzania wenzangu tatizo ni nini hasa maana takwimu hizi ni za kutisha na kusikitisha na huu ndo ujenzi wa Tanzania au ndo wapi tunaelekea?

Mdau wa Elimu.

No comments: