Saturday, February 13, 2010

maandaliz ya mwisho mwisho ya tamasha la zinduka lidaz club

Fundi Mitambo wa kampuni ya Prime Time Promotions Dj Haroun (kulia) akimwelekeza jambo mmoja wasimamizi wa tamasha hila la ZINDUKA kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na kwa wakati.Tamasha hilo linafanyika kesho katika viwanja vya Lidaz Club,kiingilio kimepangwa kuwa buku tatu kwa kila kichwa.







Pichani juu ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini ya Prime Time Promotions Ltd wakiwa bize huku na kule mchana huu kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

Pichani ni maandalizi ya tamasha kubwa la uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza malaria iliyopewa jina la "Zinduka" ambalo linafanyika hapo kesho katika viwanja vya Lidaz Club,kinondoni jijini Dar.Katika tamasha hilo mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete
litafanyika ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo.
Wasanii mbalimbali ambao wamechaguliwa kuwa mabalozi wa kampeni hiyo wataimba siku hiyo na kushirikisha wasanii wengine pia kwa pamoja ili kutoa ujumbe wenye kuhamasisha jamii kutumia vyandarua ili kujikinga na ugonjwa wa Maralia, na bbaada ya kumaliza Dar wasanii hao wataendelea na kampeni hiyo kwa nchi nzima katika kuhamasisha mapambano dhidi ya Maralia
Kampeni hiyo inaratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ikishirikiana na tasisi ya Malaria No More ya nchini Marekani ili kuhakikisha ugonjwa huo unapungua kwa kiasi kikubwa nchini kama siyo kuisha kabisa.
Baadhi ya wasanii walio saini katika uzinduzi huu wa Malaria Haikubaliki ni pamoja na; Kidumu, Diamond, Dully Sykes Marlaw, Professor Jay, Lady Jay Dee, Mwasiti, Bi Kidude, Banana Zoro, Ray C, Maunda Zoro, Tanzania House of Talent (THT) dance troupe, Banana, Amini na Pipi, Mataluma na R Tony.Tiketi za kuingia kwenye tamasha la zinduka zinauzwa kwa shilingi (3000) na zitapatikana Maduka ya Zizzou Fashions, Steers -Millenium Tower na Town Outlet.

No comments: