Saturday, February 13, 2010

MISS TZ 2009 KULA VALENTINE RUMANDE
Miss TZ 2009 Miriam gerald

Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald 22 pamoja na rafiki yake wa kiume, Kennedy Victor, jana walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kujeruhi na kuharibu mali katika ukumbi wa TPDC uliopo Mikocheni jijini Dar.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa na mwendesha mashtaka Nassor Sisiwaya mbele ya hakimu, Kweye Rusema, alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo katika ukumbi wa TPDC, Mikocheni.

Rusema alieleza mahakama kuwa tukio hilo mbali ya uharibifu wa mali, mmoja wa watu waliokuwepo ukumbini hapo, Shaban Moshi alijeruhiwa na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Mbali ya kujeruhi, vurugu hizo zilisababisha kuvunjika kwa amani na utulivu ukumbuni hapo.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka vurugu hizo zilizoanzishwa na mrembo huyo na rafiki yake na kusababisha uharibifu wa vyombo vyenye thamani ya sh. 720,000.

Baada ya kusomewa mashtaka, Hakimu Rusema alisema kuwa dhamana ipo wazi kwa watuhumiwa wote huku kila mmoja akitakiwa kujidhamini kwa 1,000,000. Hata hivyo wahusika walishindwa kujidhamini na kwenda katika mahabusu hadi Februari 25 kesi yao itakapotajwa tena.
Huyu ni mrembo wa pili kufikishwa mahakamani ambapo machi mwaka jana Miss Tanzania 2006/07 Wema Sepetu katika mahakama hiyo kwa kosa la kumfanyia vurugu mwigizaji wa filamu nchini, Steven Kanumba.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa kamti ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga wakati akizungumza na kituo cha Radio Clouds jana jioni kuhusiana na tukio hilo alikiri kupata taarifa za mrembo huyo kufikishwa mahakamani.
“Juhudi za kumuwekea dhamana zilishindikana kutokana na muda kuwa mdogo lakini juhudi zinafanyika ili siku ya jumatatu tuweze kumtoa kwa dhamana” alisema anko Hashim.

No comments: