
Kaka Kadidi,
Kwa jina naitwa Jovinata Kileo. Natokea mkoa wa Kilimanjaro. Nina miaka 28, niko single, sina mtoto, na wala sijawahi kuolewa. Baba ni Mchaga ila Mama Mjerumani. Mimi ni mtoto wa pili katika familia. ninaye Kaka ambaye ameshaoa na anaishi zake Afrika Kusini. Mama ni marehemu ila baba anaishi Moshi
Elimu ya msingi nimesomea Moshi, na baadae kujiunga na shule ya International School of Tanganyika, Kabla ya kuendelea na masomo ya Juu Afrika kusini. Nilipata shaada ya kwanza ya biashara na hatimaye ya pili ya maswala ya utawala mwaka 2005.
Kwa sasa nafanya kazi katika shirika la kuhudumia wakimbizi lililopo Juba Sudan. Ingawa ninaweza kusema kwamba nimejaliwa kazi nzuri, na maisha mazuri, ninaona upungufu Fulani maishani mwangu, kwani kila mwanamke inabidi awe na familia yake, na Muda unavyozidi kwenda, naona uzee unaninyemelea bila matumaini ya kumpata mchumba.
Nilishauriwa kwenda kwa waganga wa kienyeji ili nipata usaidizi, lakini haijasaidia. Niliyempata akawa balaa, tapeli wa kutupwa. Mmoja wa vigogo nchini aliniahidi uchumba matokeo yake nikaja kugundua ningekua mke wa tatu. Sikuwa tayari kuwa mke wa tatu. na waliokuwa wakinishauri mambo ya waganga ndo kabisa wamezalishwa na kutelekezwa.
Namtafuta kijana mcha Mungu ambaye tutakuwa pamoja. Kutokana na familia yangu kuwa ya kidini sana (walutheri) nitafurahi sana kumpata Mkristo wa aina hoyote, na pia mcha Mungu.
Manka alipoweka maombi yake ya kutafuta mchumba, wengi walimuona kama vile kichaa. Ila, katika dunia ya sasa na hali ya sasa, inambidi mwanamke atafute vigezo kwa mwanamme.Sitaki kumparamia mpiga tungi wa siku mbili tatu, wala sitaki mlevi wa ngono. Namtafuta mume ambaye atakuwa baba watoto wangu. Sitafuti makuu, namtafuta mwanamme msomi lazima hawe na masters na hawe na umri chini ya miaka 35 na ambaye hajawahi kuoa.
Mzungu marufuku, wala mtu uchanganyiko sitaki. Asiwe mlevi, au mtumiaji wa kileo cha aina yoyote. Lazima hawe na kazi, Lazima awe na roho safi , mwenye fadhila na mpenda watu atakayenipenda kwa moyo wake wote.
Ulipoiweka picha ya bwana John Mashaka mara ya kwanza, niliguswa sana, ila kwa vile sikuwa na uhakika , nilishindwa na la kufanya ili niweze kuwasiliana naye; Nilikuomba contacts na email zake lakini ukanibania. Nilipokuomba namba za Mshikaji toka Ukraine pia ulinibania, wakati alibainisha wazi kwamba naye ni single nikashindwa kukuelewa.
Ulipoibandika picha ya Mashaka hapo jana, sikuwa na budi kuchunguza zaidi ili kufahamu hali yake ya ndoa. Inshallah, hajaoa. Sitaki kujua saizi yake ya viatu, sitaki kujua ana hela ngapi au magari mangapi, simtaki kwa vile yupo Marekani . Sitaki maisha yake mazuri, ninachohitaji ni roho yake safi. Naomba kwa hisani ya mbingu unipe namna ya kuwasiliana naye ili tujuane.
Ukiona kuna ugumu, basi niunganishe na yeyote mwenye wasifu wake. Nipo Tayari kununua tiketi na hela zangu na kwenda kukutana naye popote pale alipo.
Au kama atakuja Tanzania mwaka huu, naomba unijulishe ni lini ili nikutane naye bwana Mashaka kwa ajili ya maongezi ya kawaida. Ukininyima contacts, zake, basi naomba uchapishe conctacts zangu ili kaka yeyote wa kitanzania mwenye hizo sifa anitafute kupitia
jovinatakileo@yahoo.com
WAKO MTIIFU
Jovin-Grusdin- KILEO
No comments:
Post a Comment