Friday, January 7, 2011

Nyalandu awaondolea uvivu wamachinga wa kigeni
Sokoni kariakoo shimoni wakati wa ziara
ya waziri mdogo wa biashara Mh. Nyalandu

Mh. Lazaro Nyalandu akiongea kuhusu
wamachinga wa kigeni na masoko holela jijini

Mh. Nyalandu akiangalia dagaa wa
Kigoma sokoni Kariamoo shimoni

Mh. Nyalandu akiwa ameongozana na
mstahiki meya wa Ilala Mh. Silaa


Wafanyabiashara ndogondogo ‘wamachinga’ wa kigeni wametakiwa kuondoka ndani ya siku 30 ili kuacha watanganyika kufanya biashara hizo.

Naibu Waziri wa Biashara an Viwanda, Lazaro Nyalandu alisema jana wakati alipotembela soko kuu la Kariakoo jijini Dar kuwa wageni wote kutoka nchi za Asia na Afrika wanaojihusisha na biashara hizo waache ama wafuate taratibu za uwekezaji nchini.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa wamachinga kutoka Mataifa mbalimbali ya Afrika na Asia kufanya shughuli hizo kinyume na vibali vyao,jambo ambalo linawanyima fursa wazalendo kufanya kazi hiyo.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi kwenye soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam jana,Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko,Lazaro Nyalandu alisema kuwa, idadi kubwa ya wageni hao kufanya shughuli hizo kinyume na taratibu imesababisha serikali kukosa mapato.

Alisema,kuna baadhi ya wafanyabishara wameomba kibali cha uwekezaji,badala yake wameshindwa kufanya hivyo na kuanza shughuli za umachinga huku wakiwaita ndugu zao kinyume na taratibu, kutokana na hali hiyo serikali haitawaacha, itawashughulikia.

“Wale wote wanaofanya shughuli za umachinga kinyume na vibali vyao waache mara moja na kuondoka nchini kwao kabla yakuchukuliwa hatua za kisheria, kutokana na hali hiyo watendaji weote watapita kwa kila wafanyabishara kwa ajili ya kufanya ukaguzi,”Alisema Nyalandu.

Aliongeza watanzania ambao na wenyewe wamejifanya kuwa wao ni wenyeji wa wageni hao watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ili Tanzania isionekane dampo la wafanyabiahsra wanaokwenda kinyume na sheria.

Alisema kuanzia sasa watendaji wa idara ya biashara watazunguka kwenye masoko yote kwa ajili ya kukagua vibali vya wafanya biashara hao na kuwaorodhesha ili waweze kubainika ni wa ngapi na wamekuja kufanya kazi gani.

Kwa mujibu wa Nyalandu,baadhi ya watu wanajifanya madalali wa kuwakaribisha wageni hao na kuwaingiza kwenye shughuli hizo kinyume na taratibu, jambo ambalo linasababisha serikali kukosa mapato, kutokana na hali hiyo watu hao watashughulikiwa.

Alibainisha, soko la kariakoo ni miongoni mwa maeneo yaliyojaa wageni hao, jambo ambalo limesababisha baadhi ya wazalendo kukosa nafasi ya kufanya bishara hizo.

Alibainisha,serikali kwa sasa inafanya mazungumzo na serikali ya China ili waweze kudhibiti baadhi ya wafanyabishara wasio waadilifu ambao wamekuwa wakiingiza bidhaa feki zinazohjatarisha maisha ya wananchi.

“Kuna mazungumzo kati yetu na serikali ya China kwa ajili ya kudhibiti bidhaa bandia, lengo ni kuiondoa Tanzania kuwa dampo la bidhaa hizo,kutokana na hali hiyo bidhaa zitakazokuwa zinaingia zitakuwa na ubora unaokubalika,”alibainisha.

Aliongeza kutokana na hali hiyo wananchi wanapaswa kuwa makini na wafanyabishara wa bidhaa bandia kwa akuangalia ubora wa bidhaa hizo na mahali ilipotoka.

No comments: