HATIMA YA MGOGORO WA WANAFUNZI KAMPALA INTERNATIONAL UNIVERSITY KUJULIKANA WIKI IJAYO
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi akiongea na wawakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) kilichopo nchini leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufika Ofisi ya Waziri mkuu kueleza kero zao kufuatia maandamano ya wanafunzi hao yaliyofanyika jana kupinga ongezeko kubwa la ada na kuomba wapatiwe mikopo kama vyuo vingine pamoja na kupatiwa ufafanuzi juu ya hadhi na uhalali wa Chuo hicho katika kutoa mafunzo ya elimu ya juu hapa nchini.Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) wakitoa malalamiko kwa Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi juu ya matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo mara baada ya kukutana naye leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi akisisitiza jambo na kuwatoa hofu wawakilishi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) kuhusu madai yao na kuwataka wawe watulivu wakati serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) na viongozi wa Chuo hicho watakapokutana nao wiki ijayo kutoa majibu ya matatizo yao. Juu na chini ni wawakilishi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) wakitoa malalamiko kwa Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi juu ya matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo mara baada ya kukutana naye leo jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment