Tuesday, January 11, 2011

Watu toka taasisi ambayo haukuweza julikana mara moja wakipima eneo la Coco Beach tayari kuligawa kwa jamaa ili afanye mradi wa kuchaji shilingi 1,000/- kwa kila gari.

Katika hali isiyo ya kawaida sasa wananchi watakaotaka kuja Coco Beach kupunga upepo watalazimika kujikunjua mfukoni kulipia Tshs 1,000 kwa gari kwa siku iwapo wataegesha katika maegesho yaliyopo ufukweni hapo kwenye hoteli ya Coco Beach
Ripota wa Globu ya Jamii ameshuhudia maafisa kutoka taasisi gani siuji wakipimapima eneo hilo kwa tepu, huku wakiandika andika kwenye vitabu.
Hata hivyo Wananchi waliokuwepo kwenye ufukwe huo walipinga kitendo hicho na kuwaamuru walipishaji hao kuondoka mara moja, nao wakatii maana inaonekana siku hizi Watanzania hawataki kupelekeshwa bila mpango.

Juhudi za kuwatafuta maafisa wa manispaa na watendaji wengine zinaendelea kujua uhalali wa zoezi hilo.
Uwanja unaotumiwa na watoto kucheza mpira nao ukipimwa bila shaka kwa ajili ya mradi huo wa kuchaji magari yanayokapi Coco Beach.

Wananchi wameshangazwa sana na kitendo hicho, wakikumbushia jinsi Rais Kikwete alivyowashushua madiwani wa manispaa za jiji ambao walipiga marufuku mwananchi wa kawaida kukanyaga ufukwe wa karibu na hospitali ya Aga Khan, na kuwataka wapaendeleze lakini hadi leo hakuna kinachofanyika, ingawa wananchi wa kawaida wanajinoma

"Ufukwe kwa Coco Beach ni eneo pekee lililosalia ambalo mtu wa kawaida yuko huru kwenda bila kukutana na bughudha, ikimaanisha kwamba mradi huu wa kulipisha magari hapo mahali sio tu utakera wengi ila uhalali wake lazima uthibitishwe kwa wananchi haraka sana", mwananchi mmoja alisikika akisema.

Mwinge alidakia "Hawa ndio wanaompakazia JK (Rais Kikwete) aonekane nchi ngumu kwake wakati kuna watu ambao badala ya kubuni vitu vya kufurahisha wananchi wao wanabuni vya kuwakandamiza.

Mbona Slipway kule wamemwachia mfanyabiashara ambaye kwa vile si mswahili basi anapeta atakavyo. Waache hizo na hapa hii kitu inaweza kuhatarisha usalama wa watu bial sababu. Ningekuwa na namba ya Profesa Tibaijuka ningempigia aone ardhi yake inavyotaka kuchezewa..."aliongeza.

No comments: