Wednesday, January 12, 2011


Hi Kadidi2,
Pole sana na jukumu zima la kutupasha habari za nyumbani. Hakika mdau wa Ukweli hapa na kuna mdau kutoka Urusi kanitumia hii picha kwenye akaunti ya Uso wa Kitabu na mie nikaona isiwe uchoyo tukichanga!

Aniwies hapaa inaonesha kwa jinsi gani darasani wanafunzi wake walikuwa wanafanya sana "cheating" kwa kuchunguliana na ndio wakabuni njia mpya ya JIBEBE MWENYEWE. Hahahahaha! Hahahahaha! Yaani huyu mwalimu alifanya jambo sahihi kwa kuanzisha njia hii.

Itakuwa vipi kama Mh. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akiliona hili na kulichukulia hatua kwa Elimu ya Bongo!!! Naona ugumu utazidi mara dufu! Maana duuuuh! Sipati tutafaulu wangapi miongoni mwetu! Maana kuna wale watu tunapepesa sana macho kama indiketa ya ISUZU...!!!

Ahsante sana na nakutakia kazi njema!
Mdau kutoka Solvesborg, Sweden.

No comments: