Friday, April 4, 2008
Je, Ni Kweli Harusi Zetu Zinaboa?
( Picha ya maktaba ikionyesha harusi ya kijijini kule Chala, Sumbawanga)
Kwenye moja ya picha za harusi nilizotuma juma la jana kuna mmojawetu aliyetoa maoni ambayo nadhani si vema yakapita bila kujadiliwa hapa kijijini. Mwenzetu huyu anasema;
Harusi za kiswahili utakoma ubishi mwanawane, baada ya kutiliwa shampeni kwenye glass wageni wote wanakuja kugonganisha glass zao kwenu basi hapo maharusi watasimama wee mpaka wageni wote hata kama mia tano mpaka waishe.
Ikiisha hapo kuna tena kumpa mkono wa pongezi wa pongezi bwana na bibi harusi, watasimama tena wee mpaka wageni wote watoe mkono wa pongezi, kama zawadi au kupita kumkumbatia bi harusi kumpa mkono bwana harusi. Basi mpaka wakimaliza hatua hizo kama bibi harusi amevaa mchuchumio atatamani kuvua viatu!
Lakini ndio utaratibu wetu sijui tumeotowa wapi, nashindwa kuelewa kwanini watu wakifika wasikabidhi zawadi kabisa basi mambo mengine yanaendelea. Hee hapo nimesahau kuna kusuburia zawadi za makundi, (marafiki, wafanyakazi wenzio, familia, majirani) ambao nao utasimama wee kusubiria kwanza mpaka wapigiwe wimbo wanaoutaka ndio walete zawadi.
Hata mkitoka hapo kwenda kupumzika, mnakuwa hoi hakuna shughuli yoyote itayofanyika alfajiri hiyo (maana shughuli imeisha saa nane ya usiku)ni kujimwaga kama punda! Sorry kama nitakuwa nimewakwaza lakini hata sielewi huu utaratibu tumeuiga kwa nani!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment