Ajali
*Basi la Meridian laua 8..
----------
WATU nane tisa wamekufa katika ajali mbaya iliyohusisha basi la Meridian lililokuwa likisafirisha maiti kwenda Moshi ambalo lilivaana na Toyota Hiace lililokuwa limembeba bibi harusi mtarajiwa, Bi. Stephern Hiza (22) na wapambe wake.
Katika ajali hiyo watu 12 walijeruhiwa vibaya na watu watatu kati yao kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi. Majeruhi wengine wamelazwa katika hospitali ya Bombo mkoani hapa. Dereva wa basi la Meridian alikimbia baada ya ajali hiyo kutokea na hajulikani alipo.
Watu walioshuhudia ajali hiyo waliliambia gazeti ili kuwa ilitokea juzi saa 1 usiku katika eneo la Kitumbi, Handeni. Kondakta wa Meridian , Bw. Godfrey Joseph, alisema chanzo cha ajali hiyo ni basi la kampuni moja (jina tunalo) lililokuwa likitokea Uganda kuelekea jijini Dar es Salaam kutaka kulipita lake wakati mbele kuna gari nyingine aina ya Fuso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Bw. Nyakolo Sillo, alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 1 usiku, wakati dereva wa Meridian alipogonga kwa nyuma gari aina Toyota Hiace.
Waliokufa katika ajali hiyo mbali na bibi harusi mtarajiwa ni Latipha Undole (1), Neema Cheddy (26), mkazi wa Kawe, Stephern Hiza (11) ambaye ni mdogo wake na marehemu bibi harusi mtarajiwa na mwanafunzi wa darasa la tano Zuberi Mohamed (35).Wengine ni Joseph Matunda (23), mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambaye ni mkazi wa Namanga, mwanamke aliyefahamika kwa jina la moja la Mama Maswapu mkazi wa Mbagala na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Mariam.
Maiti zimehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali Teule ya Bombo, Tanga na majeruhi wamelazwa hospitalini hapo. Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabara, Bw. James Kombe, ambaye alikuwepo katika eneo la tukio alisema wahusika waliosababisha ajali hiyo watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, ametuma salama za pole kwa wale wote waliopata msiba.
No comments:
Post a Comment