Monday, August 23, 2010

wasanii wapendezesha mkutano wa kampeni wa JK, wafurahia msimamo wake wa kuwasaidia
Ankal akiwa na mdau Eric David Nampesya wa BBC wakiendeleza libeneke
Baadhi ya wasanii wakiwa nyuma ya jukwaa kabla ya kunda mmoja mmoja kuburudisha

Sir Juma Nature na watu wake wakighani mistari

Chege (shoto) na Mheshimiwa Temba wakiwajibika mbele ya maelefu ya wakazi wa Mwanza wakati wa mkutano wa kampeni wa JK Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza



Msanii Diamond akifanya vitu vyake

Pailkuwa hapatoshi
Wasanii waliotoa burudani katika picha ya pamoja baada ya kupeana mikono na JK ambaye hakuficha kusema kwamba yeye ni mpenzi sana wa Bongo Fleva na kwamba ingawa hachezi anasikiliza sana midundo yao na ameahidi kuwasaidia. Kwanza ameshaleta mtambo wa kisasa wa kurekodia na kufanya mixing wenye thamani ya dola elfu 50, amewapatia nyumba ya studio na wataalamu wa kufundisha mainjinia wa sauti wako njiani. Vile vile ametoa milioni 20 kuwapatia wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuandaa mkakati wa jinsi ya kuwasaidia wasanii wa muziki na filamu kuwa na uwezo wa kusambaza kazi zao na kupata faida ya kuvuna jasho lao, badala ya hali ilivyo sasa ambapo wafanyabiashara wanatawala soko na kuacha wasanii wakiumia na wachache kuneemeka kwa kazi zao
Msanii Dokii (kijani) akiwa na kundi la Flora Mbasha ambalo lilitia fora sana kwenye mkutano huu wa kampeni






No comments: