Friday, August 13, 2010

Dodoma Jana.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho kushoto, akizungumza jambo na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Nje ya ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Mjini Dodoma jana, baada ya kuaghirishwa kwa kikao hicho hadi leo asubuhi. Katikati ni Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, kulia Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Zakia Hamdani Meghji.
Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa na Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati hiyo ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma Jana, kabla ya kuaghirishwa kwa kikao hicho hadi Leo asubuhi.

No comments: