Tuesday, August 3, 2010

Kocha wa Brazil Achinja Mastaa

Kocha mpya wa Brazil, Mano Menezes ametaja majina ya wachezaji 24 watakaocheza mechi ya kirafiki na Marekani mwezi ujao. Maicon, Lucio, Kaka na Fabiano, ambao wamepumzishwa wakati Ronaldo, De lima na Ronaldho Gaucho wamejumuishwa licha ya kutemwa awali na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Dunga kwenye michuano ya kombe la Dunia.

Katika kikosi hicho mshambulaji wa Ac millan Alexenda Pato ameitwa kikosini licha ya kutoswa na Dunga. "Tuna matumaini ya kutengeneza kikosi kizuri zaidi. Kazi iliopo mbele ni ngumu lakini hatuna budi kuifanya" alisema Menezes.

Rais wa shirikisho la soka Brazil [C.B.F] Ricardo Teixeira alisema "Tunaamini uwezo wa kocha huyu na tumekubaliana naye kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kikosi cha mwaka 2014."

Brazil itakuwa wenyeji wa fainali wa kombe la Dunia 2014.

No comments: