
Wadau Picha juu ni mtoto Samuel Emanuel Nkya na athari ya tukio la kuungua kwa dawa alipokuwa akitibiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili. Hivi sasa, Samuel ana miaka minne na nusu na anatarajiwa kuondoka nchini mapema mwezi huu kwenda India, kufanyiwa marekebisho ya eneo lililoathirika ikiwa ni upasuaji wa awamu ya pili.Tunaomba dua zenu Mungu amjalie apone na kufurahi na watoto wenzake.

Mtoto Samuel Emanuel,akiwa na Kamati ya maandalizi ya tiba yake inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi huu nchini India.Kutoka kushoto ni Athumani Hamisi, Emanuel Nkya, David Sawe na Muhidin Issa Michuzi.Picha na habari hii kwa msaada mkubwa wa Globa Publishers Limited.
No comments:
Post a Comment