Monday, September 13, 2010

VODACOM MISS TANZANIA YAFIKIA TAMATI….!!!

Toka habari zianze kurindima katika vyombo vya habari nchini yapata mwezi sasa na tumekuwa tukiwaona katika shughuli mbalimbali za kijamii hatimaye kiu ya wapenzi wa shindano hili ilikidhiwa usiku wa kuamkia tahere 12/9/2010 katika viwanja vya Mlimani City ndani ya wilaya ya Kinondoni.

Mshindi toka Wilaya ya Temeke Genevieve Emmanuel Bila ya kuamini masikio yake alitajwa kuwa mrithi na mmliki mpya wa taji la Miss Tanzania 2010.

Usiku huo kila kitu kilikuwa katika mpangilio ambao ulidhihirisha ukomavu wetu katika kutayarisha matukio makubwa. Umati mkubwa wa wageni mbalimbali toka nchi tofauti ulikuwa mashahidi wakuu ndani usiku huo kama hukubahatika kushuhudia usisikitike sana na kama ujuavyo asili yetu tunakuletea yote yaliyojiri katika picha zenye ubora wa hali ya juu..

Karibuni Sana..!

Vodacom Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel (katikati) akiwa na washindi wenzake mara baada ya kutangazwa mshindi kwenye shindano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi (kulia) ni mshindi wa tatu Consolata Lukosi na (kushoto) ni mshindi wa pili Glory Mwanga.

Warembo walioshiriki kwenye shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakitoa shoo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa utambulisho.

Baadhi ya majaji wakifuatilia shindano kwa ukaribu sana.

My world running low…!!! ni maneno ya Mwanadada Wahu kutoka nchini Kenya(kulia) akiimba sambamba na Mwanamuziki Chege Chigunda(katikati) huku wakipewa Back Up na Mh. Temba wakati wa Onyesho la Vodacom Miss Tanzania likiendelea.

Washiriki wakipita jukwaani Kujitambulisha kwa wageni waalikwa na kunadi sera zao.

Vijana wa THT wakitoa burudani kwa wageni waliofika kushuhudia Onyesho hilo.

Washiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiwa jukwaani na Vazi la Ufukweni.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. William Lukuvi (mwenye miwani) akifuatilia kwa umakini shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010.

Washiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakipita kwa pamoja jukwaani na Vazi la Jioni.

Washiriki waliofanikiwa kuingia kwenye 10 bora za Vodacom Miss Tanzania 2010.

Hawa ndio 5 bora za Vodacom Miss Tanzania 2010.

Wadau mbalimbali wakifuarilia Shindano la Vodacom Miss Tanzania kwa umakini zaidi.

Mzee wa Commercial AY akitoa mchango wake kwenye Vodacom Miss Tanzania 2010.

Shukrani za dhati na Mo Blog.

No comments: