HII SASA SAFI…..!!!!
Askari wa usalama barabarani wakiwa wametapaka maeneo ya mkabala na jengo la IPS kuhakikisha magari yaliyoegeshwa maeneo yasiyo rasmi kuondolewa.
***********************
Katika pitapita ya kuangalia jinsi hali ya foleni katika maeneo mbalimbali inasababishwa na nini leo asubuhi katika jiji la Dar es Salaam maeneo ya Posta karibu na Keep left cha askari monument imekutana na wingi wa askari wa usalama barabarani wakijaribu kuondoa magari katika maeneo yasiyo ya parking za magari.
Tukio hilo limefanyika kwa mda mchache tu na baadaye kuonyesha kuwa uwekaji holela wa magari husababisha foleni katika maeneo mbalimbali.
Lakini hii isiwe ni katikati ya jiji tu hata pembezoni mwa jiji itumike na ikiwezekana kila anayeingia na gari katikati ya mji awe analipia kiasi cha 20,000Tsh itakayosaidia kupunguza msongamano wa magari katikati ya mji na hata kwenye barabara zetu.
Askari wa usalama barabarani akijaribu kuita magari yaliyosabanisha foleni kabla ya zoezi zima la kundoa magari yaliyoegeshwa maeneo yasiyo rasmi.
Wafanyakazi wa gari aina ya Break down wakishughulika kwa kasi kutekeleza wajibu wao wa kuondoa magari yaliyoegeshwa sehemu zisizo rasmi kama amri ya askari.
Gari aina ya Prado lennye namba za Usajili T 728 AQQ likiondolewa na break down,lakini sisi hatujui linakoelekea….!!!
No comments:
Post a Comment