Wednesday, September 15, 2010

taarifa ya kukosekana kwa maji jijini dar

DAWASCO inawatangazia wateja wake katika baadhi ya maeneo kwamba,kutakuwa na zoezi la kubadilisha Valve katika Matenki ya Terminal yaliyopo maeneo ya Chuo Kikuu.

TAREHE; 17 -18 /09/ 2010.

MUDA ;Siku mbili (2)

SABABU; Ubadilishwaji wa valve zilizochakaa na kuweka mpya.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA; Ni pamoja na chuo cha ardhi, chuo kikuu cha Dar es Salaam,Lugalo(sehemu ya jeshi) Mlimani City,Mlalakua,(Survey) Coka cola,Sinza,eneo la Sam Nujoma, sehemu ya Ubungo,(NHC) Mabibo,Kigogo,Buguruni pamoja na maeneo ya jirani.

DAWASCO inawaomba wananchi wa maeneo hayo yaliotajwa kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi katika kipindi hicho ambacho matengenezo yatakua yanaendelea na hivyo kusababisha upungufu wa maji kwa muda wa siku hizo mbili.

Huduma ya maji itarejea katika hali yake ya kawaida baada ya muda huo.

DAWASCO inawaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Isaidie DAWASCO kwa kutoa taarifa za uvujaji na kwa kulipa bili yako ya maji kila mwezi ili iweze kutoa huduma bora jijini.

DAWASCO

Tutakufikia.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
DAWASCO
Simu:0762979627

No comments: