Tuesday, September 14, 2010

Leseni mpya za udereva wa magari kuzinduliwa kesho
Mkurugenzi wa huduma kwa mlipa kodi, Mamlaka ya Mapato (TRA), Protas Mmanda, akionyesha mfano wa leseni mpya za udereva, makao makuu ya TRA jijini Dar. Shoto ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Polisi wa usalama barabarani, Johansen Kahatano. Habari na www.wavuti.com
Picha na Chachandu Daily blog.


Mamlaka ya mapato Tanzania, TRA, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini wameanza utekelezaji wa mfumo mpya wa utoaji leseni za udereva wa vyombo vya moto kwa lengo la kudhibiti ajali za barabarani na utoaji holela wa leseni na kudhibiti mapato ya Serikali.

Kadhalika, Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Polisi wa Usalama Barabarani, Johansen Katahano, amesema kuwa madaraja ya leseni hizo yameongezwa kutoka 8 hadi 14. Madaraja hayo yameongezwa katika daraja A na C na yameongezwa kutokanana na uwezo wa vyombo vya moto vya madaraja husika na idadi ya abiria watakaobebwa na vyombo hivyo.

Uzinduzi wa matumizi wa leseni hiyo yatafanyika
kesho Jumatano jijini Dar.

Leseni hizo mpya zitakuwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu za kielektroniki za mtumiaji ikiwemo idadi ya makosa aliyoyafanya akiendesha chombo cha moto, gari na pikipiki.

Leseni hizi mpya zitahitimisha matumizi ya leseni za zamani.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Protas Mmanda amewataka madereva wanaotumia leseni zao za kawaida kutokuwa na wasiwasi kwani kwa muda huu wataendelea kutumia leseni hizo kihalali na watapewa leseni mpya watakapokuwa wanakwenda kwa ajili ya kuzihaishi. Watu wenye leseni za Daraja C wataanza kupata leseni hizo mara moja lakini watahitajika kupata mafunzo maalumu kwanza.




No comments: