Wednesday, September 22, 2010

IBADA YA KUAGA MWILI WA ALIEKUWA MKEMIA MKUU WA SERIKALI
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. John Magufuli akitoa heshima za mwisho wakati wa ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Dk. Ernest Mashimba aliyekuwa Mkemia Mkuu wa Serikali kabla ya kusafirishwa kwenda Mwanza kwa Mazishi katika Kijiji cha Ngudu wilayani Kwimba.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Aisha Kigoda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Ernest Mashimba nyumbani kwake mtaa wa Ursino, Regent Estate, Dar es Salaam.
Mke wa aliekuwa Mkemia Mkuu wa Serikali Marehemu Ernest Mashimba mama Rose Ernest akisaidiwa na ndugu wakati alipopita mbele ya jeneza la marehemu mume wake wakati wa kuaga mwili wa marehemu nyumbani kwake jijini Dar es salaam, mwili wa Marehemu mashimba umesafirishwa Jana kwenda kijiji cha Ngudu Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza kwa mazishi. Marehemu Ernest Mashimba alifariki wiki iliyopita Mkoani kwenye hoteli ya Executive Inn Lushoto mkoani Tanga alikokwenda kwenye mahafali ya mtoto wake Happy Ernest aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari ya Kifungiro mkoani humo.
Mtoto wa Marehemu aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari ya Kifungiro mkoani Tanga Happy Ernest Mashimba akiuaga mwili wa marehemu baba yake kwa majonzi makubwa.

No comments: