Monday, September 6, 2010

maajabu ya makaburi kando ya barabara ya iringa
Nyaya na nguzo za umeme zikiwa zimekata denge kuepuka kupita juu ya makaburi yaliyo kando ya barabara kuu kilomita chache toka Iringa ukitokea Mbeya. Kuna hadithi zinasema Tanesco walishindwa kupitisha nyaya hizo juu ya hayo makaburi kwa sababu ambazo awali hazikuwa zinafahamika. Kuna hadithi zingine pia zilidai kwamba ukipiga picha hapo huwa hazitoki
Makaburi hayo kama yanavyoonekana yakiwa kandoni mwa barabara
Katika pitapita zake ankal alibahatika kuwakuta mafundi wa Tanesco wakiwa kazini karibu na eneo hilo. aliposimama na kuwauliza, na baada ya kusitasita kidogo, mmoja wa mafundi hao alijitolea kwa kumwambia ankal kwamba waliepa kupitisha nyaya hizo juu ya makaburi hayo kuepuka gharama ambayo wangepata bila shaka kwa kulipa fidia katika kuyahamisha. Bahati mbaya hapakuwa na mkaazi wa eneo hilo ili kutoa ufafanuzi. Hivyo kama kuna mdau mwenye data tunaomba msaada tutani ili wadau wapate mwanga halisi wa maajabu haya...

No comments: