Wednesday, April 30, 2008
Mchawi Mwingine aliyebambwa Tabata Huyu Hapa !!
Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Rehema Kefa (18) akiwasilisi katika Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar es Salaam,baada ya kukamatwa akiwa katika Zahanati moja iliyoko Tabata akiwa katika harakati za kutafuta mtoto na kunywa damu yake.Msichana huyo,alikamatwa na kuwekwa chini ya uangalizi wa polisi,baada ya kukiri kuwa ameanza kufanya kazi zinazodaiwa kuwa ni za kichawi akiwa na miaka mitano.
---------
Siku tatu tu baada ya kijana kukamatwa na kichwa cha mtoto, kijana mwingine, safari hii msichana, amekamatwa katika hospitali ya Tabata iliyopo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar kwa tuhuma za kutaka kuiba mtoto wodini.
Rehema Kefa(18) Mkazi wa Mkuranga alikutwa akitaka kumtorosha mtoto huyo leo aliyekuwa katika wodi ya mateniti hospitalini hapo leo.
Inasemekana Rehema alibambwa na nesi wa zamu katika wodi hiyo ambaye ni mlokole, ambaye baada ya kuona mauzauza ya huyo msichana inasemekana alifanya maombi, na mtuhumiwa huyo akaanza kutambaa kama nyoka wodini hapo.
Polisi waliitwa na kumpeleka Rehema kituo kidogo kilichopo karibu na hospitali hiyo ambako alikiri kwamba yeye ni mtu wa juju, na kudai kwamba shughuli hiyo kafundishwa na bibi yake kwa jina la Salome Nganame.
Aliwaambia askari kwamba hakuwa peke yake katika skuli hiyo, kwani mafunzo hayo ya undondocha kafunzwa yeye na kinadada wengine aliowataja kama Asha Said(29), Fatuma Saleh(23) na Khadija Mpogolo.
Alisema yeye na hao aliowataja ilikuwa waibe pamoja mtoto pele hospitali na kwenda kumnyonya damu.
aliwaambia askari kwamba walipomkamata bibi huyo na wenzie walikuwa wanawacheki tu kwenye 'TV' yao huko waliko.Picha na Mpiga Picha Maalum wa TSN.
Breaking News..
Matokeo ya Urais Zimbabwe
Tsvangirai 47%,
Mugabe 43%
Pichani ni Kiongozi Mkuu wa chama cha Upinzani nchini Zimbabwe(MDC) Morgan Tsvangirai akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya Matokeo Ya uchaguzi yaliyorudiwa
kuhesabiwa kwa mara ya pili kumpa ushindi wa 47% na kumpita Mpinzani wake Mkuu Rais Wa sasa Robert Mugabe Kutoka chama cha ZANU-PF aliyeambulia 43%
Tsvangirai 47%,
Mugabe 43%
Pichani ni Kiongozi Mkuu wa chama cha Upinzani nchini Zimbabwe(MDC) Morgan Tsvangirai akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya Matokeo Ya uchaguzi yaliyorudiwa
kuhesabiwa kwa mara ya pili kumpa ushindi wa 47% na kumpita Mpinzani wake Mkuu Rais Wa sasa Robert Mugabe Kutoka chama cha ZANU-PF aliyeambulia 43%
Da' Chemi..
Ronaldo Azua Balaa..
Pichani ni Carla mmoja wa walimfanyia varangati Ronaldo akitoa maelezo Polisi huku mwenzie Andrea akiwa Ndani ya gari.
-----------
Mchezaji mahiri wa kimataifa wa Brasil Ronaldo amepatikana na janga jingine kuhusiana na ukware, Ronaldo amepigana na "malaya" watatu alioingia nao kwenye chumba cha Motel yake baada ya kugundua kuwa hawakuwa wanawake bali ni wanaume waliojibadilisha kuwa wanawake (pichani juu)
Waziri Mkuu Pinda awasili Iringa ...
Rais Kikwete akutana na Tsvangirai..
HUYU NI MDAU WA BLOG YA HAKUNAKULALA!!!
Ebwana huyu ni Albert, mdau mwenzangu wa blog,yeye ni mmiliki wa blog ya www.hakunakulala.blogspot.com...na pia ni mpenzi wa Bwawa la maini kama anko Michuzi asemavyo jana nae alikuwa na furaha pia baada ya bwawa lamaaini kufanya mambo pale London nae anasema kama mshabiki namba one wa Bwawa la maini hakuna wa kuwazuia kuchukua kikombe safari hii !!!
Mdau Emma asherekea !!!
KERO UBUNGO KIBANGU
KAKA Safari,
NACHUKUA FURSA HII KUWAWAKILISHA WATU WA UBUNGO WENZANGU KUELEZA KILIO CHETU JUU YA HILI BONDE UNALOLIONA.
HILO BONDE KABLA HALIJAFIKIA HALI HIYO LIMESHAWEKEWA VIKAO SI CHINI YA KUMI KUWACHANGISHA WANA UBUNGO WOTE, NA SISI RAIA KWA KUPENDA MAENDELEO TUKAITIKIA WITO WA SERIKALI YETU YA KIJIJI TUKACHANGA'TENA NA TENA. 'LAKINI KAKA MICHUZI, AMINI USIAMINI, TANGU TUCHANGE ZAIDI YA MARA 7 HAKUNA HATA KIPANDE CHA KOKOTO KILICHOWEKWA KWA BONDE HILO MPAKA LIMEFIKA HATUA HIYO.
SASA WATU WA KUKAMATA MAFISADI WASIKAMATE HUKO JUU TU WAJE NA HUKU VICHOCHORONI. WAPO' MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA UBUNGO KIBANGU NA DIWANI WAKE WAHOJIWE KUHUSU FEDHA ZA MICHANGO ZA HAPA.
MDAU
UBUNGO KIBANGU
wamejileta wenyeeeeewe moscow...
mdau atunisha mchango kwa mtoto samweli Nkya !!
samweli
mdau meshack mfugale akabidhi dola 500 kwa emmanuel nkya kama mchango wake kwa mtoto samwel nkya (pichani juu) anayehitaji kwenda india kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na matibabu katika uso wake ambao umeharibika. walioshuhudia ni wajumbe wa kamati ya kumsaidia mtoto samweli akatibiwe.
mdau mfugale anayefanya kazi darfur, sudan, ni mmoja ya wadau wengi waliojitokeza kumchaangia mtoto huyu kiasi sasa mchango umetimia dola 9,500 na zimebakia dola 2,500 tu kukamilisha matakwa yote ikiwa ni pamoja na tiketi ya ndege mtoto samwel na baba yake, matibabu na malazi hospitali mwezi mmoja.
Baba wa mtoto huyo, emmanuel nkya, ametoa shukrani sana kwa wasamaria wema wote waliochangia kwa hali na mali. safari ya kwenda india inatarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia sasa.
Rais Kikwete ateta na Wafanyakazi, AU..
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wa Pili kulia,akiongea wafanyakazi katika Makao Makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa Ehiopia leo.Kushoto ni Mwenyekiti mpya wa Kamisheni ya Umoja huo,Jean Ping na kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania Bernard Membe.Rais Kikwete,anatarajiwa kukutana na Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika.
Baadhi ya watumishi wanaofanya kazi katika Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) iliyopo jijini Addis Ababa Ethiopia wakimsikiliza kwa Makini Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa anaongea nao jan katika Makao makuu ya umoja huo Addis Abba Ethiopia.
tenda ya mkutano wa sullivan kwa wenye benz !!
MDAU,
ENDAPO KAMA UNA GARI AINA YA MERCEDES BENZ , RANGI NYEUSI AMA NAVY BLUE MUUNDO WA E200, E250, E300 NA E500 NA IKO KWENYE HALI NZURI WASILIANA NA KITENGO CHA SULLIVAN WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA AMBACHO KINAKUSUDIA KUKODISHA MAGARI AINA YA MERCEDES BENZ SALOON KWA MUDA WA SIKU 10 KUANZIA MEI 28, 2008 HAD JUNI 6, 2008 KWA AJILI YA MKUTANO WA SULLIVAN UTAOFANYIKA ARUSHA KATI YA JUNI 2 HADI 6. 2008.
PELEKA GARI LAKO KWA UKAGUZI GOVERNMENT TRANSPORT AGENCY (GTA) PALE BOHARI KUU BARABARA YA NYERERE KUANZIA MEI 3, 2008 KATI YA SAA MBILI UNUSU ASUBUHI NA SAA TISA UNUSU ALASIRI.
KITENGO CHA SULLIVAN TANZANIA KITAKODISHA GARI LAKO KWA GHARAMA ISIYOZIDI SHILINGI 150,000/- KWA SIKU.
KWA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NA KITENGO CHA SULLIVAN SIMU NAMBA
022 2111906/11,
2110185,
2128336,
AMA
0787 245424,
0715 599 299
KWA HABARI ZAIDI JUU YA MKUTANO WA SULLIVAN
http://www.thesullivansummit.go.tz/
Tigo Lotto..
hasheem aamua kusaka nondozz zaidi
Connecticut center Hasheem Thabeet plans to return to school for his junior season instead of entering the NBA draft.
The 7-foot-3 native of Dar es Salaam, Tanzania, was projected as a first-round pick in the draft.
Thabeet averaged more than 10 points and almost eight rebounds a game as a sophomore, and ranked third in the nation with 147 blocked shots. He was the Big East's defensive player of the year, helping UConn to a 24-9 record.
"As a team, we took a step in the right direction this year, but I look forward to us working together to win a Big East Championship and making a run at a national championship," Thabeet said in a statement released Sunday by UConn. "I really enjoy being here, getting a great education and spending time with my friends and teammates."
Thabeet, 21, has been playing organized basketball for fewer than six years.
"Hasheem has made as much progress as any player I have coached in my 36 years and if he continues that incredible progress, he will help us take the next step as a team and help himself become one of the best players in college basketball," UConn coach Jim Calhoun said.
Filamu zinazowania tuzo za Vinara 2007/08..
-----------
Filamu zilizoingizwa na watengenezaji wa filamu nchini kuwania tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania 2007/2008 2007/2008 (Vinara Film Awards), zimetajwa.
Katika taarifa kutoka mratibu wa One Game Promotion inayoaandaa tuzo hizo, Khadija Khalili, iliyotumwa kwenye vyombo vya habari zaidi ya filamu sabini zinawania tuzo hizo.
Taarifa hiyo ilizitaja filamu hizo kuwa ni Crying Silently (Kilio Moyoni), Kolelo, Mwanahiti, Zawadi ya Fisadi, Oloboni na Layoni, Mmera (Jando) na Nyamaume.
Nyingine ni Sumu ya Moyo, Segito, A Point of no Return I, A Point of no Return II, Dar to Lagos, Cross my Sin na Penina.
Pia zimo Habari Kubwa, Fake Pastor, Chite Ukae, Surprise, Stranger, Fungu la Kukosa, Sea Man, Mzee wa Chabo, Donda Ndugu, I Love You, Miss Bongo I, Miss Bongo II, Revenge, Behind the Scene, na My Wife.
Taarifa hiyo ilizitaja nyingine kuwa ni My Sisters I, My Sisters II, Machozi ya Nyamoma, Silent Killer, My Wife, Greena, Kiapo cha Damu, Valentine, Mwana Pango, Utata, Yolanda, Picnic, Uwanja wa Dhambi, Misukosuko II, Copy, Lugha Gongana, Mtoto wa Mjini, Nyuma ya Pazia, Macho Mekundu, Tanzia, Welcome Back, Karibu Paradiso, Swahiba, The Game of Love I, The Game of Love II na The Game of Love III.
Nyingine ni Mahabati, Security, Itunyama, The Body Guard, Agano la Urithi, Ndani ya Gereza, Simu ya Kifo, My Heart, Malipo ya Kisasi I, Malipo ya Kisasi II, Mpasuko wa Moyo I, Mpasuko wa Moyo II, Kisasi na Diversion of Love.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa, majaji watakutana wiki ijayo kuanza kuziangalia tuzo hizo.
Taarifa hiyo ilisema kuwa filamu zinazowania tuzo hizo ni zile zilizokamilika kutengenezwa Januari 2007 mpaka Machi 31, 2008.
Vipengele vinavyoangaliwa na majaji katika filamu hizo ni Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Muongozaji Sinema Bora wa Mwaka, Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu na Mtunzi Bora wa Filamu.
Vingine ni Filamu Bora ya Kutisha, Muigizaji Mwandamizi Bora wa kike (supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike, Adui Bora kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa Filamu ambao wote watapata tuzo na zawadi.
Pia itatolewa tuzo ya heshima kwa wale waliotoa mchango wao kukuza sanaa nchini.
Tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Mei zimedhaminiwa na bia ya Ndovu Special Malt, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Global Publishers.
Filamu zilizoingizwa na watengenezaji wa filamu nchini kuwania tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania 2007/2008 2007/2008 (Vinara Film Awards), zimetajwa.
Katika taarifa kutoka mratibu wa One Game Promotion inayoaandaa tuzo hizo, Khadija Khalili, iliyotumwa kwenye vyombo vya habari zaidi ya filamu sabini zinawania tuzo hizo.
Taarifa hiyo ilizitaja filamu hizo kuwa ni Crying Silently (Kilio Moyoni), Kolelo, Mwanahiti, Zawadi ya Fisadi, Oloboni na Layoni, Mmera (Jando) na Nyamaume.
Nyingine ni Sumu ya Moyo, Segito, A Point of no Return I, A Point of no Return II, Dar to Lagos, Cross my Sin na Penina.
Pia zimo Habari Kubwa, Fake Pastor, Chite Ukae, Surprise, Stranger, Fungu la Kukosa, Sea Man, Mzee wa Chabo, Donda Ndugu, I Love You, Miss Bongo I, Miss Bongo II, Revenge, Behind the Scene, na My Wife.
Taarifa hiyo ilizitaja nyingine kuwa ni My Sisters I, My Sisters II, Machozi ya Nyamoma, Silent Killer, My Wife, Greena, Kiapo cha Damu, Valentine, Mwana Pango, Utata, Yolanda, Picnic, Uwanja wa Dhambi, Misukosuko II, Copy, Lugha Gongana, Mtoto wa Mjini, Nyuma ya Pazia, Macho Mekundu, Tanzia, Welcome Back, Karibu Paradiso, Swahiba, The Game of Love I, The Game of Love II na The Game of Love III.
Nyingine ni Mahabati, Security, Itunyama, The Body Guard, Agano la Urithi, Ndani ya Gereza, Simu ya Kifo, My Heart, Malipo ya Kisasi I, Malipo ya Kisasi II, Mpasuko wa Moyo I, Mpasuko wa Moyo II, Kisasi na Diversion of Love.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa, majaji watakutana wiki ijayo kuanza kuziangalia tuzo hizo.
Taarifa hiyo ilisema kuwa filamu zinazowania tuzo hizo ni zile zilizokamilika kutengenezwa Januari 2007 mpaka Machi 31, 2008.
Vipengele vinavyoangaliwa na majaji katika filamu hizo ni Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Muongozaji Sinema Bora wa Mwaka, Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu na Mtunzi Bora wa Filamu.
Vingine ni Filamu Bora ya Kutisha, Muigizaji Mwandamizi Bora wa kike (supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike, Adui Bora kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa Filamu ambao wote watapata tuzo na zawadi.
Pia itatolewa tuzo ya heshima kwa wale waliotoa mchango wao kukuza sanaa nchini.
Tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Mei zimedhaminiwa na bia ya Ndovu Special Malt, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Global Publishers.
Tuesday, April 29, 2008
Mazishi Ya Mtoto Salome..
Upendo Danstan, mama mzazi wa, Salome Yohana,aliyechinjwa na mtuhumiwa Ramadhani Mussa wiki iliyopita,akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu mwanawe, aliyezikwa katika makaburi ya Segerea jijini Dar es Salaam leo.
Wazazi wa Salome Yohana aliyekutwa amekufa siku ya Jumamosi na baadae kichwa chake kukutwa kikinyonywa damu juzi na Ramadhani Mussa,wakizika mwili wa mtoto wao leo jioni kwenye Makaburi ya Segerea jijini Dar es Salaam
Sehemu ya Umati wa waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni kabla ya kuelekea kwenye Mazishi ya Mtoto Salome (3) aliyezikwa leo kwenye Makaburi ya Segerea jijini Dar es Salaam,Mwenyezi mungu ailaze roho ya Marehemu Salome mahala pema peponi Ameni.Picha Zote kwa Msaada Mkubwa wa Mpoki Bukuku The Citizen na Bernard Rwebangira kutoka TSN.
Uchaguzi Chuo Kikuu
KUTOKUWEPO kwa jina la mgombea urais wa serikali ya wanafunzi (DARUSO) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Odong’ Odwar raia wa Uganda aliyekuwa akikubalika na wanachuo walio wengi, baada ya jina lake kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho kwa madai kuwa hakuwa na sifa ya kuwa chuoni hapo kimesababisha wanafunzi wengi kususia uchaguzi huo.
Pamoja na wanafunzi wengi kususia uchaguzi ila wachache waliojitokeza kupiga kura waliongozwa na wasichana, huku wavulana wengi wakionekana kuvinjari sehemu mbalimbali katika vituo vya kupigia kura chuoni hapo bila kupiga kura.Hata hivyo ilielezwa kuwa sababu kubwa iliyofanya wavinjari katika vituo hivyo ni kuwabainisha wenzao ambao walidhaniwa kuwa wangekaidi na kusaliti msimamo wao.
Mwitikio wa uchaguzi haukuwa mkubwa baada ya wapiga kura wengi kukataa kupiga kura kwa kile walichodai kuwa mgombea waliyekuwa wanamtaka hakuwepo hivyo hawakuwa na sababu ya kupiga kura kumchagua mtu asiye chaguo lao.Hata hivyo kulikuwa na kampeni ya chinichini chuoni hapo iliyolenga kuzua wanafunzi kutopiga kura ingawa baadhi yao walionekana wakivinjari katika vituo vya kupigia kura bila kupiga kura.Habarii hii na Jackson Odoyo na Christopher Maregesi.
Undani zaidi Juu ya Kifo Cha Mtoto Salome..
Pichani juu ni kijana Ramadhani Mussa (12)ambae anashikiliwa na polisi Mkoa wa Ilala kwa kukutwa na kichwa cha mtoto mdogo Salome Yohana (3) alichokuwa amekibeba katika mfuko wa rambo kwenye hospital ya taifa ya muhimbili Hivi karibuni.
Picha juu kulia aliposimama Mdau,ni sehemu inayoaminika kuwa mtoto
Salome alichinjwa..
---------
Mauaji ya kikatili ya kuchinjwa kama kuku mtoto pekee kwa wazazi wake, Salome Yohana (3) yameumiza wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam na hata nje ya jiji na vitongoji vyake na wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali wote waliohusika na kitendo hicho.
Akimsimulia mwandishi wetu jinsi Salome alivyotoweka nyumbani na kukutwa amechinjwa, mama mzazi wa mtoto huyo, Upendo Dustan (27) alisema kuwa siku hiyo ya Ijumaa wiki iliyopita majira ya saa 2.00 usiku aliandaa chakula wakala na mwanaye ambaye baadaye alikwenda kucheza nje na mtoto wa jirani yao.
ohooooo...kumbe kufungwa kubaya...
Wachezaji wa Man u jana wliafanya bonge la vagi baada ya kukataa kutoka uwanjani mpira ulipoisha jana. Inaonyesha iliwauma vibaya sana kipigo cha jana mpaka wakashindwa kujibihev. kwa maelezo zaidi leo wanapambana na Barcelona yatatokea haya muamuzi ni dakika 90 na pia namwambia muheshimiwa Fisi akae chonjo maana na hao wapinzani wa bwawa la maini kama kaka michuzi asemavyo nao wanahitaji ushindi ndio utamu ulipo hapo !!!
gym ikila vumbi
Mambo ya Precision Air !!
mwaitege kukiaga chama cha ukapera
Muimbaji maarufu wa nyimbo za injili Bony Mwaitege aliyetamba sana na wimbo wa UTANITAMBUAJE KAMA NIMEOKOKA,anatarajia kufunga ndoa mapema julai mwaka huu,aidha habari zinasema kuwa tayari amemvisha pete ya uchumba Bi Subiraga Mwasaga katika kanisa la E.A.G.T Mito ya Baraka jijini Dar-es-salaam.kwa habari zaidi mdau ingia strictlygospel.wordpress.com
Yu wapi Balali !!
Mtoto aliyekatwa kichwa azikwa Leo..
Pichani Ramadhani Mussa (12)ambae anashikiliwa na polisi Mkoa wa Ilala kwa kukutwa na kichwa cha mtoto mdogo Salome Yohana (3) alichokuwa amekibeba katika mfuko wa rambo
kwenye hospital ya tIafa ya muhimbili Hivi karibuni.Kwa sasa bado anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi..
----------
MTOTO Solome Majana (3) aliyefariki wiki iliyopita katika mazingira ya kutatanisha baada ya kichwa chake kutenganishwa na kiwiliwili chake amezikwa leo makaburi ya Tabata. Akizungumza na majira jana baba wa mtoto huyo, Bw. Yohana Majana (26),alisema wamekamilisha taratibu zote za kipolisi na waliruhusiwa kuchukua mwili huo wakati wowote kuanzia jana asubuhi.
"Tumemaliza taratibu zote za polisi na leo (jana asubuhi) tulikubaliana kuwa muda wowote tukiwa tayari tuuchukue mwili wa marehemu kwa maziko, tumeruhusiwa kufanya hivyo."alisema Akizungumzia mkasa huo alisema serikali inatakiwa kuamini kuwa uchawi upo na watu wanaobainika kuhusika katika matukio ya kichawi kama lililomtokea kwa mwanae Salome, wawajibishwe.
Bw. Majana, alisema yapo matukio mengi ambayo yanatokea ambayo yanahusika na masuala ya uchawi lakini kutokana na Serikali kutotilia mambo yamekuwa yakienda hivi hivi na watu wengi kuathirika. Alisema mtoto wao Salome alitoweka nyumbani Aprili 25 mwaka huu jioni na kesho yake walikuta mwili wake ukiwa umekatwa kichwa.Habari hii na Eben-Ezery Mende
Pole Mactemba kwa Moto !! (Bamaga)
Mmiliki wa blog ya mactemba.blogspot.com jana alipata pigo la kuunguliwa na mahali anapoishi Maeneo ya bamaga pia ule moto wajana uliteketeza malizake zote na kumrudisha hatua nyuma. Mimi na wadau wote tuna mpa pole sana na Mungu amsaidie aweze kusimama tena najua Mzee wa tatu bila au Mzee wa Epa Mungu atakujalia na utarudi kama zamani. Kwa msisitizo na rudia kukupa Pole sana wewe na laazizi wako mimi kama mmiliki na wadau wote wa hii blogu wako pamoja na wewe katika wakati huu mgumu !!
LONDON SCHOOL OF COMMERCE ..
Ndugu wananchi (wadau), Chuo cha LONDON SCHOOL OF COMMERCE (associate college of university of wales) kinatangaza usajili maalumu wa wanafunzi wapya wa mwaka huu wa masomo 2008/9 unaoanza mwezi wa sita (June) 2008.
Kwa taarifa zaidi na kozi mbalimbali wanazotoa tembelea tovuti yake www.lsclondon.co.uk .Kuna punguzo maalumu la Ada kutoka £6450 mpaka £3950 kwa mwaka wa masomo huu kwa wanafunzi wa kitanzania watakaopitia kwangu kuomba na kukubaliwa masomo yao hapa chuoni, punguzo hili maalumu utalipata kwa kuwasiliana nami ili nikuwakilishe hapo chuoni.
Naomba wanafunzi wenye interest na kusoma chuoni hapa kwa kozi zilizotangazwa kwenye tovuti ya chuo tuwasiliane kwa namba yangu hii hapa +447506458289.... au email hii (ally.abdallah@lsclondon.co.uk).... Natoa tahadhari kwamba Mimi ni wakala wa wanafunzi wa kitanzania ninayehusika na punguzo la bei tu.
Sihusiki kabisa na upatikanaji wa kibali cha kuingilia Nchini (visa), kwahiyo naomba nisiulizwe maswali kuhusu swala hilo,chuo kitakamilisha kila taratibu za mwanafunzi aliyekubaliwa masomo na kupata nafasi chuoni ili eweze kupata visa..
kwa maelezo zaidi kuhusu upatikanaji wa visa za uingereza bofya hapa http://www.ukvisas.gov.uk/en/Ni matarajio yangu, kila mwenye kutaka kupata habari zaidi za kusoma chuoni hapa na punguzo hili la bei atapitia tovuti ya chuo kwanza ili kumaliza mushkeli aliokuwa nao, kisha kuwasiliana na mimi ili kupata punguzo hilo la ada.
NB: unapowasiliana nami tafadhali nukuu jina la chuo kwanza LSC halaf endelea na ujumbe, maswali.. nk.. yako.
TAHADHARI: Sitopokea malipo kutoka kwa mwanafunzi yeyote yule,ada na malipo mengine yanafanyika katika kitengo husika chuoni, ili upate punguzo ni kuwasiliana na mimi nikupe taratibu hisika.
Asanteni
Kwa taarifa zaidi na kozi mbalimbali wanazotoa tembelea tovuti yake www.lsclondon.co.uk .Kuna punguzo maalumu la Ada kutoka £6450 mpaka £3950 kwa mwaka wa masomo huu kwa wanafunzi wa kitanzania watakaopitia kwangu kuomba na kukubaliwa masomo yao hapa chuoni, punguzo hili maalumu utalipata kwa kuwasiliana nami ili nikuwakilishe hapo chuoni.
Naomba wanafunzi wenye interest na kusoma chuoni hapa kwa kozi zilizotangazwa kwenye tovuti ya chuo tuwasiliane kwa namba yangu hii hapa +447506458289.... au email hii (ally.abdallah@lsclondon.co.uk).... Natoa tahadhari kwamba Mimi ni wakala wa wanafunzi wa kitanzania ninayehusika na punguzo la bei tu.
Sihusiki kabisa na upatikanaji wa kibali cha kuingilia Nchini (visa), kwahiyo naomba nisiulizwe maswali kuhusu swala hilo,chuo kitakamilisha kila taratibu za mwanafunzi aliyekubaliwa masomo na kupata nafasi chuoni ili eweze kupata visa..
kwa maelezo zaidi kuhusu upatikanaji wa visa za uingereza bofya hapa http://www.ukvisas.gov.uk/en/Ni matarajio yangu, kila mwenye kutaka kupata habari zaidi za kusoma chuoni hapa na punguzo hili la bei atapitia tovuti ya chuo kwanza ili kumaliza mushkeli aliokuwa nao, kisha kuwasiliana na mimi ili kupata punguzo hilo la ada.
NB: unapowasiliana nami tafadhali nukuu jina la chuo kwanza LSC halaf endelea na ujumbe, maswali.. nk.. yako.
TAHADHARI: Sitopokea malipo kutoka kwa mwanafunzi yeyote yule,ada na malipo mengine yanafanyika katika kitengo husika chuoni, ili upate punguzo ni kuwasiliana na mimi nikupe taratibu hisika.
Asanteni
Nyumba yateketea kwa Moto Sinza..
Moto mkubwa ambao chanzo chake inadaiwa kuwa shoti ya umeme ukiteketeza nyumba ya Bi Aisha Issa muda mfupi uliyopita maeneo ya Sinza Bamaga, katika tukio hilo Kikosi cha Zimamoto kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kilishindwa kuzima moto huo baada ya gari kugoma kutoa maji na hivyo wananchi kulazimika kujaribu kuuzima kwa kutumia ndoo! Hii ndiyo hali halisi ya 'Faya' zetu za Bongo! Picha na Christopher Lissa
Mafua ya Kuku Janga la Taifa..
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akishuhudia wakati Kuku akitolewa damu kwa ajili ya kupimwa kama ana maambukizi ya ugonjwa wa mafua makali ya ndege,katika sherehe ya uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Tahadhali na Udhibiti wa ugonjwa huo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana.Kulia ni Dk. Chanasa Mpelumbe-Ngeleja kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kushoto ni,Mfugaji wa Kuku Bi Stella Chambo na katikati ni Waziri wa mifugo na uvuvi Mh John Pombe Magufuli.Picha Ofisi ya Waziri Mkuu
------------
SERIKALI imeutangaza ugonjwa wa mafua ya ndege kuwa ni moja ya majanga ya kitaifa yanayoikabili nchi.
Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akizindua mpango tahadhari na udhibiti wa ugonjwa wa mafua ya ndege nchini, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
"Baada ya kutambua tishio la ugonjwa huu ni kubwa na lina athari kubwa, serikali imeamua kutangaza ugonjwa huu ni moja ya majanga ya kitaifa. Kwa maana hiyo serikali imeamua kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na ugonjwa huo," alisisitiza Pinda.
Waziri Mkuu Pinda alisema kuna uwezekano mkubwa wa ugonjwa huo kuingia nchini kwa kuwa tayari umeenea Kusini mwa nchi ya Sudan.Habari hii na James Magai
Mzee Mzima Bozi Boziana Kuwasha Moto Bongo..
Mratibu wa Tamasha la uzinduzi wa albamu mpya ya Akudo Impact a.k.a wazee wa masauti, Bahati Sigh(katikati)akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa albamu ya Impact yenye jumla ya nyimbo nane itakayo zinduliwa Mei 16 ndani ya ukumbi wa diamond jubilee.katika uzinduzi huo pia kutakuwepo na vikundi vya utangulizi kama Jahazi Modern Taarab pamoja na mwanamuziki aliyewahi kuwika sana miaka ya nyuma kutoka Congo (DRC) Mzee Mzima Bozi Boziana
MATOKEO YA KURA ZA MAONI..
Fichueni Mafisadi -Rais Kikwete
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa Ikulu, Bw Salvator Rweyemamu akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ikulu jana jijini Dar es Salaam juu ya ziara ya Rais Jakaya Kikwete kuelekea nchini Ethiopia na Uganda kutekeleza majukumu yake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
katika Mazungumzo hayo na waandishi wa Habari Bw Rweyemamu alisema Rais Jakaya Kikwete amewataka wafanyakazi nchini,kukataa kutumika katika miradi ya mafisadi na vigogo wa rushwa ili kuwafanya vigogo hao washindwe kutimiza malengo yao. alisema badala yake Rais amewataka wafanyakazi kuwa mstari wa mbele katika kuwafichua vigogo hao bila woga.
Alisema iwapo wafanyakazi watagoma kutumikishwa katika `madili` ya kifisadi na rushwa, itakuwa vigumu kwa vinara wa mambo hayo kufanikisha matendo hayo maovu.
Katika kuwapa moyo wafanyakazi hasa wakati huu wanapojiandaa kusherehekea SikuKuu yao ya Mei Mosi, Bw. Rweyemamu alisema Rais Kikwete amefurahishwa mno na kauli mbiu ya mwaka huu inayosema`Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana Mafisadi wakitokomezwa'.Kutokana na hilo,Rais amewataka wafanyakazi wawe mstari wa mbele katika mapambano ya kutokomeza rushwa na ufisadi.
`Rais anawaomba wafanyakazi, viongozi na wananchi kwa ujumla washirikiane na Serikali katika mapambano haya,`alisema Bw Rweyamamu kwa niaba ya Rais.Habari hii na Simon Mhina,Picha Mrocky
National Staff Day..
Jean ping M/kiti Mpya wa Kamisheni AU..
Mwenyekiti wa Umoja wa Africa (AU) na Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwenyekiti wa kamisheni ya umoja wa afrika (AU) aliyemaliza muda wake profesa alpha oumar konare ambaye leo kakabidhi madaraka hayo kwa Mh. Jean Ping addisababa Ethiopia.
Mwenyekiti wa Umoja wa Africa (AU) na Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia makabidhiano rasmi kutoka kwa mwenyekiti wa kamisheni ya umoja wa mataifa aliyemaliza muda wake Alpha Oumar Konare(kushoto) kwenda kwa Mwenyekiti Mpya wa kamisheni hiyo Mr.Jean Ping kwenye makao makuu ya Umoja wa Africa,Addis Ababa Ethiopia mchana jana.
Rostam Azizi alishitaki Gazeti la Mwana Halisi..
MFANYABIASHARA maarufu nchini,Rostam Azizi Pichani,amemshitaki Mhariri wa gazeti la kila wiki la MwanaHalisi na wachapishaji wake akitaka alipwe Sh bilioni tatu kwa kuchapisha habari zinazomkashifu zikimhusisha pamoja na mambo mengine, kashfa ya Kampuni ya Richmond.
Rostam ambaye pia ni Mbunge wa Igunga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amefungua kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wiki iliyopita, akimtumia wakili Kennedy Fungamtama. Licha ya kutaka alipwe kiasi hicho cha fedha, Mbunge huyo pia anaiomba Mahakama kutoa amri ya muda kulizuia gazeti hilo, wakala wake au yeyote kuchapisha habari zinazomkashifu.
Zaidi ya hayo, mfanyabiashara huyo ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Kamati Kuu, anaiomba Mahakama iliamuru gazeti hilo kumwomba radhi kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti hilo kwa uzito uleule au zaidi baada ya hukumu yake.
Pia anaomba alipwe gharama za kesi. Rostam anadai kuwa gazeti hilo la MwanaHalisi lilichapisha habari za uongo na za kumkashifu katika toleo lake namba 084 la Februari 13 hadi 19, mwaka huu, chini ya kichwa cha habari, “Richmond ya Rostam Azizi, Ndiye aliyeileta nchini.” Kulingana na mfanyabiashara huyo, kichwa hicho cha habari pamoja na habari yenyewe, zinaonyesha kuwa yeye ni mdanganyifu, asiye mwaminifu, mtoa rushwa na anayetenda matendo maovu na mtu anayeshiriki katika mambo ya udanganyifu.
Rostam anadai kuwa licha ya kuweza kupatikana kwa taarifa sahihi na za wazi kwa urahisi na kwamba kwa njia yoyote ile hajashiriki katika matendo hayo maovu, gazeti hilo liliendelea na kampeni chafu dhidi yake katika toleo lake la 085 la Februari 20 hadi 26, mwaka huu. Anadai kuwa gazeti hilo linadaiwa kuchapisha habari nyingine kwenye ukurasa wa pili chini ya kichwa cha habari, “Kikwete amtosa Lowassa” likimhusisha na biashara zake na kampuni yake, kwamba ni mtu anayefahamika kwamba anaweza kubadilisha ukweli kukidhi matakwa yake.
Mbunge huyo analituhumu gazeti hilo kuendelea kuchapisha habari kama hizo katika toleo lake la 087 la Machi 5 hadi 11, mwaka huu na toleo la 093 la Aprili 16 hadi 22, mwaka huu likimwonyesha kuwa si mtu muadilifu na anatumia vibaya nafasi yake kwa maslahi yake binafsi. Mfanyabiashara huyo analalamika kuwa maneno hayo yalikuwa na nia ya kumchafua katika biashara na kazi yake kama Mbunge; hivyo kuharibu wasifu, tabia, uadilifu na hadhi yake na kuonyeshwa kwenye jamii kuwa ni mtu wa kashfa, asiye na maana na mdanganyifu.
Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, amejijengea hadhi kama raia mwema, mfanyabiashara, mwanasiasa na mtu wa kuaminika kwa miaka mingi na kutokana na kashfa hiyo, amevunjiwa hadhi mbele ya jamii. Mbunge huyo amedai kuwa anastahili kulipwa kutokana na udhalilishaji huo kwani hadhi yake imeshushwa kiasi cha kuathiri biashara na kazi yake kwa kiwango cha kushindwa kuendesha kazi na biashara yake kwa urahisi.Habari hii na Faustine Kapama.Picha na Salum Mnette
Siku Ya Taifa..
Mzee Ruksa..
Ridhwan..
Monday, April 28, 2008
Uchimbaji Haramu wa Mchanga...
Gazeti la ThisDay linaripoti kwamba ile tabia ya uchimbaji haramu wa mchanga pembezoni Mwa Barabara kuu ya Bagamoyo (Mbezi) umerudi kwa kasi ya aina yake kama muonavyo pichani,kwani eneo hilo lilipigwa marufuku na serikali kuchimbwa agizo ambalo lilitolewa na waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa.Lakini hivi mpaka sasa hakuna mamlaka yoyote inayotilia umakini wa eneo hilo..
Subscribe to:
Posts (Atom)