Wednesday, January 21, 2009



RTO-IRINGA ISIWE NGUVU YA SODA

Mhariri,

NAFURAHI kusema kwamba nimefurahishwa na RTO-Iringa bwana Mnubi ambaye kama sijakosea ni senior superitendant kicheo.Bwana huyu juzi tarehe 19/01/ 09 alitusimamisha pale Iringa{check point} na kuanza kukagua magari yote yanayosafiri mikoa ya jirani kupitia mkoa wake.Akishirikiana na vijana wake pamoja na mkaguzi wa magari wa polisi wa mkoa,walikagua kama kila gari lina dereva wa ziada pia kama linakidhi mahitaji ya kusafiri safari ndefu,kwa magari ambayo hayakukidhi sheria hizo yalitozwa faini ya shilingi laki moja kama faini au kumwacha kondakta apelekwe kortini na wengine kuruhusiwa kuendelea na safari.

Kwa kitendo hicho kililaaniwa na abiria wengi wakiwemo wa basi nililokuamo HOOD la Tunduma wakidai kwamba wanacheleweshwa bila kujua kwamba RTO na timu yake wako kazini pia wako pale pia kulinda haki ya abiria na kupunguza ajali barabarani cha kushangaza ni kwamba abiria wa basi langu na mabasi mengine walianza kumzomea na kumtukana RTO wakisahau haki yao ya kufika salama,ni muhimu madereva kupokezana hasa kwa safari ndefu kwani siyo nzuri kiafya pia umakini barabarani unapungua kwa sababu akiwa mmoja anachoka.

Binafsi naunga mkono kazi ya RTO-Iringa ila TU ISIWE NGUVU YA SODA.Kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza ajali barabarani natoa rai abiria tusiwe tunatetea upumbavu unaofanywa na madereva kama waliofanya basi nililokuamo na mengine.Pia vita ya kupunguza ajali si ya askari polisi tu bali na abiria pia kwani wao ndiyo walengwa wakuu.

Hii iwe changamoto kwa ma RTO wengine kwani kutokua kwao makini kunawapa kiburi madereva na madereva wanamwona RTO –Iringa mnoko wakati yuko kazini.Chakushangaza tulitoka Dar,Pwani na Morogoro lakini hatukukaguliwa hii inanipa picha ya UZEMBE wa ma RTO wa mikoa hiyo.Hivyo pongezi kwa RTO-Iringa na timu yake, pia Iringa iwe ni mfano ,

kwani mabasi hubeba roho za watu na si mawe.

Kasuga (mzee wa muliko),


No comments: