Thursday, January 29, 2009
mkubwa fella aja na singo yake kuleta heshima
Anaitwa Said Fella lakini unaweza ukaanza kumuita kwa jila la Mkubwa Fella nae bila hiyana huitika kwa bashasha kabisa.Kwa wale wasiomfahamu vyema ni yule meneja wa kundi la Wanaume TMK Familly lenye makao yake makuu kule kule Temeke jijini Dar.
Mkubwa Fella amenitonya hivi punde kwa njia ya simu kwamba ameingia studio ya Sound Crafterz kwa ajili ya kurekodi singo yake ya kwanza itakayoitwa 2009.Amesema kuwa anataka kuwaonesha baadhi wasanii ambao wamekuwa wakimfuata wakati wa shida na kusaidiwa, wakishiba wanakuja na maneno ya kashfa na kiburi kama baadhi ya wasanii wengine ambao wamekuwa wakimtuhumu kwa maneno ya hapa na pale.
"Nataka kuwaonesha baadhi wasanii kuwa hata mimi na naweza,ili kuthibitisha hilo wakae mkao wa kula nakuja na singo yangu ya kwanza itakayoitwa 2009, sasa nipo studio ya Sound Cfafters kwa ajili kurekodi hiyo singo,ambayo anaamini itawashtua wengi,kwamba aalahh hata Mkubwa Fella anaweza"alibainisha Mkubwa Fella
nakuja na mambo mapya-Steve Nyerere
Steve Nyerere akiwa kwenye maandalizi makubwa ya kipindi chake ambacho kitahusisha mchakato mzima unaoizunguka jamii pamoja na wageni waalikwa ambao watakuwa wakichangia mada hizo kwa namna moja ama nyingine
Shoto ni Boss wa HATMAN PRODUCTIONS pamoja na mwanamuziki wa FM Academia Patchou Mwamba wakivutiwa na uandaaji wa kipindi cha Steve Nyerere talk show kitakachoanza kurushwa hewani mwezi ujao na televisheni ya TBC 1 jijini Dar
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini maandalizi makubwa ya kipindi cha Steve Nyerere talk show
Steve akimuigiza Rais Jakaya Kikwete wakati wa maandalizi ya kipindi chake
Msanii mchekeshaji na muigizaji wa sauti mbalimbali za watu maarufu ajulikanae kwa jina la Steve Nyerere akimuigiza Rais JK katika moja ya hotuba zake,hayo ni moja ya maandalizi makubwa na ya kufa mtu ya utengenezaji wa kipindi chake kitakachoitwa Steve Nyerere Talk Show kitakachokuwa kinarushwa na televisheni ya TBC hapa jijini Dar.Kipindi hicho kinachorekodiwa na kampuni ya HATMAN PRODUCTIONS kinatarajiwa kuanza kurushwa hewani mwezi ujao,haya wadau kaeni mkao wa kula mambo mapya yanakuja TBC.
NB: Ukimuhitaji Steve Nyerere katika shughuli zako mbalimbali wala usisite bofya namba hii 0715 782424 na utasikilizwa na kujibiwa haraka.
Askari wa JWTZ amuogesha dereva wa school bus
hivyo japo haionekani vizuri:-
"Kaka naomba uiwakilishe hii picha ya askari wa JWTZ aliyemuogesha
dereva wa school bus pale kawe darajani kwa komba asubuhi ya leo baada
ya kumwagia maji viatu vyake ambavyo anadai alivipiga kiwi leo asubuhi.
Haya sio ya kusikia nimeyaona kwa macho na watu wadau wengine pia
alishuhudia. Hebu tuulize wana jamii; Mlinzi wa wananchi anapofanya kitu
hii wewe unapata picha gani?" Nawakilisha
NB:Wadau mimi kama kawaida yangu ya ujumbe,si mnajua mjumbe hauwawigi
Wednesday, January 28, 2009
Nimekutumia hii picha niliyoipiga hivi punde, ili na wadau wengine wajionee Bongo isivyo tambarare.
Ni wiki mbili tu zimepita tangu ajali itokee huko Tanga kwa basi kuligonga nyuma lori lililokuwa limeharibika, pasi kuwa na vielelezo vyovyote kuwa limesimama kwa ubovu, na wala hapakuwa na reflectors nyuma ya lori hilo.
Hebu tazama hili gari ya takataka, hapa niliibamba ikikata kona, kutoka barabara ya M/nyamala kuingia Kawawa, indiketa zake hazifanyi kazi, taa za nyuma hata moja haiwaki, kibao cha namba hakipo, na huu wavu waliozuia nao uchafu unavujisha kidogo kidogo, thus uchafu ulikuw aunadondoka barabarani. Pia tairi zake kipara wakati limebeba mzigo mzito namna hii.
Swali; Hii inamaanisha traffic hawalioni? Au mnaliona na huwenda hawaruhusiwi kulikamata? au huwenda ndio linavyotakiwa kuwa kiuchafuuchafu?, au hili lori liue watanzania wangapi ndio mpate pa kuanzia kuchukua hatua ili tuione mnafachapa kazi?
Imagine gari kama hilo mdau linapata breakdown usiku, alafu unakuja nyuma yake itakuwaje? Natumai kama mhishimiwa fulani angekuwa na maono kuwa baada ya siku kadhaa gari yake ingejibamiza hapo nyuma ya hii lori, maamuzi yake ya leo yangekuwa tofauti.Au angekuwa na maono kuwa school bus alilopanda mtoto wake italivaa lori hili kwa nyuma, angechukua hatua flani leo. Kwakuwa haya yoote hatuwezi kuwajua ni bora kuchukua hatua leo.
Mdau MG
( Koplo wa polisi jamii)
Soma stori nzima kwa
Survival for the fittest....!!!!
Ndo maisha yalivyo....hususan kwa wanyama wasio na utashi......... mbabe ndo anaendelea kula hewa ya hii dunia......!!! sio lazima iwe porini tu.... ata uraiani....!!!Tuesday, January 27, 2009
Mnaokuja Dom muwe macho....!!!
Eneo la mlima uliyopo dodoma makulu ambapo alimanusura matapeli watatu wawili kutoka dsm wakiwa na mwenyeji wao wamlize babu wa watu kutoka rombo kiasi cha sh40m...fedha ambayo babu huyo aliipata baada ya kuuza nyumba yake iliyopo dsm.... hata hivyo polisi mkoani dom walistukia game na kumwokoa babu huyo asitapeliwe......Eneo hili ndilo babu huyo toka rombo alipoambiwa kuwa atazungumza na babu anayeweza fanya mazingara chapaa hizo Sh40m zikawa Sh600m.....
Hapa kuna mishumaa pamoja na udi ambayo huwashwa na kumpumbaza mtapeliwa kuwa ataongea na maruhani.... ila kwa mbele kama anapoelekea kamanda mmoja pichani kuna tundu la kutokea upande wa pili.... ila kwa juu yake kuna madondora kichizi.....!!!
Beware!
WIZI ULIONIKUTA
Kuna kijana ambaye anadai ametoka Morogoro na ametumwa na mzee wake kununua gari kumbe ni taperi na mwizi .
Kwa kadiri ya wiki mbili kijana alikuwa akifuatilia Gari ambayo nilikuwa naiuza na nikaitangaza katika Dar – Advert . Alisema yakuwa yeye yuko Morogoro na anahitaji kuiona gari ; mnamo tarehe 25 / 12 / 2008 asubuhi , tulipokea simu yakuwa tukutane na kijana ambaye ameondoka morogoro tumuuzie hilo gari . ( Na mpigaji akiwa ni mzee wake kutoka Morogoro; baada ya muda kijana aliomba udhuru ya kuwa tarehe 25 ni Krismasi baba yake angependa aje kuangalia hilo gari ila yeye hataweza atafika tarehe 26 / 12 / 2008 .
Saa moja asubuhi tarehe 26/12/08 alipiga simu na tukaelewana tukutane naye B.P petrol station Mbezi Beach ..tulipokutana alicheki gari kama mnunuzi yeyote kutoka bodi mpaka engine.akaomba afanye road test –he is a good driver
Alionyesha kuridhika na gari na kuonyesha nia ya kulipia fedha ambayo alikiri iko kwa jamaa ya baba yake aliyepo jmall ambaye ni agent wa oilcom.; alipotoka j mall alidai amepewa fedha ambayo ni dollar hivyo ilibidi tuende mlimani city kubadili fedha na kudeposit kwenye account kwani anasisitiza hapendi kulipana fedha mkononi angependa tulipane bank.
Tulipokuwa ndani ya bureau de change alikuwa akiwasiliana na jamaa zake na simu yake ilizima kwa kukosa chaji hivyo aliomba simu yangu kwa mawasiliano pia alielezea juu ya hali yake kuwa amekunywa dawa amoxyline na tumbo linamsumbua kwani hajapata kifungua kinywa hivyo angependa kwenda kuchukua maziwa hivyo alitoka nje huku akiwasiliana kwa kutumia simu yangu.
Kwa vile nilishakaa naye kwa muda upatao masaa matatu na juu ya yote alikuwa ameacha bahasha yake ya dollars tulipokuwa tumekaa sikupata wasiwasi naye kabisa.
Alipotoka ndani tu katika dakika tano nilishuku hivyo nikafungua bahasha yake kuchungulia mzigo wa dolla nikakuta ni magazeti yaliyofungwa vizuri haikuchukua dakika kumi watu ambao contact zao zilikuwa ndani ya simu yangu walipokea message iliyosomeka ifuatavyo
“ naomba unitumie vocha ya 5000/= nitakurudishia niko sehemu hapana duka na nahitaji sasa hivi”
Watu wengi waliibiwa kupitia kutumtumia dolla.
Ninawataarifu jambo hili kwani nimegundua limemtokea na mwenzangu ofisini siku ya jumapili 21/12/08 na mimi nilituma dolla nikifikiri namsaidia kumbe naibiwa. Kwa huyu mwenzangu mbinu iliyotumika ni sawa kabisa na mbinu iliyotumika kwangu.nina wasiwasi wengi watalizwa na kijana huyu.
Kijana ni smart, knowledgeable, polite looking, courageous na kimwili ni mdogo mdogo and very friendly during the discussions si rahisi kumshuku
Kinachonisikitisha kijana yuko bright laiti angalitumia hizi sifa zake kufanya kazi rasmi naamini angekuwa mbali sana
Haya …bomu hilo kaeni macho!!!!!!peleka ujumbe huu kwa watu wowote utakaoweza ili kupunguza tatizo.
Kumbe hii ndio bahi….!!
Mbuzi aliyekuwa akila ride juu ya kichwa cha scania akiangalia mandhari ya bahi wakati lori
MADEREVA BWANA.... NOMA KICHIZI....!!!!
Haya sasa.... huyu naye tena anamdraiv mheshimiwa... ila angalia alipoegesha gari.....!!!!Huyu naye baada ya kumwaga mchanga.... tipa limekataa kurejea sehemu yake.... akaamua kutambaa hivyo hivyo.... huku deiwaka wake akiwa nyuma kimashakamashaka....!!!
Mwingine kaamua tu kudharau ishara ya barabarani (kushoto) inayomwonyesha kuwa hiyo ni njia moja tu.... hairuhusu gari kuenda upande anaoelekea...........!!!!
MADEREVA BWANA.... NOMA KICHIZI....!!!!
Haya sasa.... huyu naye tena anamdraiv mheshimiwa... ila angalia alipoegesha gari.....!!!!Huyu naye baada ya kumwaga mchanga.... tipa limekataa kurejea sehemu yake.... akaamua kutambaa hivyo hivyo.... huku deiwaka wake akiwa nyuma kimashakamashaka....!!!
Mwingine kaamua tu kudharau ishara ya barabarani (kushoto) inayomwonyesha kuwa hiyo ni njia moja tu.... hairuhusu gari kuenda upande anaoelelea...........!!!!
Vichwa TRL kweli vimechoka....!!!! Kumbe ndo maana enz za mwl waliitaga gari moshi...!!!
Injini ya treni ikitoka stesheni ya dom njiani kuelekea bara..... kilichonivutia ni hali ya utoaji moshi mwingi mno..... hii ni moja kati ya uchafuzi wa hali ya hewa........!!!BORA ATCL IONDOKANA NA HAYA....!!!
Bila huruma ya sirikali.... Any Time Canceled Limited ingewafika haya.....!!!Watoto wa mitaani ni tatizo kichizi dom
Kijana aishie katika mazingira magumu akiwa amelala katika bustani ya Nyerere mjini
Wednesday, January 21, 2009
RTO-IRINGA ISIWE NGUVU YA SODA
Mhariri,
NAFURAHI kusema kwamba nimefurahishwa na RTO-Iringa bwana Mnubi ambaye kama sijakosea ni senior superitendant kicheo.Bwana huyu juzi tarehe 19/01/ 09 alitusimamisha pale Iringa{check point} na kuanza kukagua magari yote yanayosafiri mikoa ya jirani kupitia mkoa wake.Akishirikiana na vijana wake pamoja na mkaguzi wa magari wa polisi wa mkoa,walikagua kama kila gari lina dereva wa ziada pia kama linakidhi mahitaji ya kusafiri safari ndefu,kwa magari ambayo hayakukidhi sheria hizo yalitozwa faini ya shilingi laki moja kama faini au kumwacha kondakta apelekwe kortini na wengine kuruhusiwa kuendelea na safari.
Kwa kitendo hicho kililaaniwa na abiria wengi wakiwemo wa basi nililokuamo HOOD la Tunduma wakidai kwamba wanacheleweshwa bila kujua kwamba RTO na timu yake wako kazini pia wako pale pia kulinda haki ya abiria na kupunguza ajali barabarani cha kushangaza ni kwamba abiria wa basi langu na mabasi mengine walianza kumzomea na kumtukana RTO wakisahau haki yao ya kufika salama,ni muhimu madereva kupokezana hasa kwa safari ndefu kwani siyo nzuri kiafya pia umakini barabarani unapungua kwa sababu akiwa mmoja anachoka.
Binafsi naunga mkono kazi ya RTO-Iringa ila TU ISIWE NGUVU YA SODA.Kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza ajali barabarani natoa rai abiria tusiwe tunatetea upumbavu unaofanywa na madereva kama waliofanya basi nililokuamo na mengine.Pia vita ya kupunguza ajali si ya askari polisi tu bali na abiria pia kwani wao ndiyo walengwa wakuu.
Hii iwe changamoto kwa ma RTO wengine kwani kutokua kwao makini kunawapa kiburi madereva na madereva wanamwona RTO –Iringa mnoko wakati yuko kazini.Chakushangaza tulitoka Dar,Pwani na Morogoro lakini hatukukaguliwa hii inanipa picha ya UZEMBE wa ma RTO wa mikoa hiyo.Hivyo pongezi kwa RTO-Iringa na timu yake, pia Iringa iwe ni mfano ,
kwani mabasi hubeba roho za watu na si mawe.
Kasuga (mzee wa muliko),
Tuesday, January 20, 2009
Delphina Kasuga .
Wajukuu zako tunakukumbuka sana Ronald Kasuga, Fina Kasuga ,Joshua Kasuga, Rose Lema, Ferald Akyoo, Magdalena Akyoo, Safari Kawa, Agustino Kasuga, Babu na wengineo wengi neo wengi ulioshirikia na nao kwa ukaribu .
Tutakukumbuka Daima .
Raha ya milele umpe Ee Bwana na mwanga wa milele Umwangazie Astarehe kwa Amani Amina .
Monday, January 19, 2009
tarehe 12 ndio walitanagaza rasmi kuvunja ndoa na vyama vingine vya upinzani!!
SOURCE: Nipashe
Saturday, January 3, 2009
UTAMU WATOWEKA MBEYA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetupilia mbali rufaa ya mgombea wa Chadema kupinga kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Mbeya Vijijini. Mgombea wa Chadema, Sambwee Shitambala (pichani aliyenyanyua vidole vya ushindi)alienguliwa na Tume ya Uchaguzi ya Mbeya Vijijini baada ya vyama vya CCM na CUF kuwasilisha pingamizi, vikidai kuwa alikiuka Sheria ya Uchaguzi kwa kuapa kwa wakili badala ya kwa hakimu.Mgombea huyo ambaye ni mwanasheria, hakukubaliana na uamuzi huo na kukata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Lakini leo, mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Lewis Makame aliwaambia waandishi wa habari kwenye hoteli ya Mount Livingstone kuwa baada ya kutafakari mambo makuu manne, tume yake imetupilia mbali rufaa hiyo.