Thursday, July 24, 2008

Toleo La Raia Mwema Wiki Hiii
*EPA sasa ni kitendawili.
WINGU limetanda kuhusu hatima ya uchunguzi wa wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutokana na kwamba muda wa uchunguzi umepita lakini hakuna taarifa rasmi iliyokwisha kutangazwa juu ya uchunguzi umebaini nini.
Akitangaza kuanzishwa kwa uchunguzi huo, Januari mwaka huu, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, alisema kwamba Tume aliyounda Rais Jakaya Kikwete kuchunguza EPA ikiongozwa na Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Said Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dk. Edward Hosea, ingechukua miezi sita, ambayo ilimalizika Julai 9.Kwa mengi zaidi juu ya Habari hiii na Makala mbalimbali ikiwemo Rai ya Jenerai Ulimwengu Bofya na Endelea....>>>>>>

No comments: