Thursday, July 24, 2008

msiba: Mzee thomas marijani kizigha katutoka
Ibada maalum kumuombea Mzee Thomas Marijani Kizigha leokatika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front jijini kabla ya kupelekwa uwanja wa ndege tayari kwa kusafirishwa kesho asubuhi
Msafara ukianza toka nyumbani kwa mtoto mkubwa wa marehemu, Charles Kizigha, Mbezi Beach
Mwandishi Mwandamizi wa Tanzania Standard Newspapers Ltd (TSN) wachapishaji wa gazeti la daily News na HabariLeo, Charles Kizigha, akiwa amebeba msalaba baada ya Ibada maalum ya kumuombea Marehemu Baba yake mzazi, Mzee Thomas Marijani Kizigha ambaye anatarajiwa kuzikwa wiki hii nyumbani kwao Usangi mkoani Kilimanjaro. Imepangwa asafirishwe kesho kwa ndege Jeneza lilolobeba mwili wa marehemu likiingizwa kanisani kwa ibada maalum
waombolezaji wakiwa kanisani
Kaka Franklin Mziray akiteta jambo na mfiwa Charles Kizigha
Baadhi ya wafanyakazi wenzie na Charles Kizigha wakiwa kanisani na waombolezaji wengine
Familia ya Hayati Mzee Thomas Marijani Kizigha kanisani leo


No comments: