Wednesday, July 30, 2008

Sumaye Atoa Siri....
Sumaye Atoa Siri....

WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ametoboa siri nzito ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa,jinsi alivyomteua mara mbili kuwa waziri mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwa waziri mkuu pekee aliyelitumikia taifa kwa mihula miwili mfululizo.

Sambamba na hilo,Sumaye alisema kwa jinsi mambo yanavyokwenda nchini, anamshukuru Mungu kwamba alishindwa katika Uchaguzi Mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano.
Sumaye alisema hayo juzi katika mahojiano maalumu na kipindi cha ‘Jicho Letu’ wiki hii, kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Clouds FM.Mahojiano hayo ya Sumaye, yanatarajiwa kurushwa na kipindi hicho Jumamosi ijayo.

Bila kufafanua kwa undani,Sumaye alisisitiza kuwa kwa jinsi hali ya mambo inavyokwenda kiuchumi,kisiasa na kijamii,hajutii kabisa kuikosa nafasi hiyo iliyokutanisha wagombea wengine 11 kutoka Chama Cha Mapinduzi(CCM)na hatimaye Rais Jakaya Mrisho Kikwete,kuibuka mshindi.

Katika mahojiano hayo,Sumaye alitoboa siri ya mshituko alioupata siku alipoitwa na Rais mstaafu Mkapa,na kujulishwa nia ya kutaka kumteua ili awe waziri mkuu.‘‘Kusema ukweli, sikuwa na habari hadi saa 7:30 ya siku ya uteuzi,ndipo Rais Mkapa aliponidokeza nia yake ya kutaka niwe waziri mkuu.Sikutegemea wala sikuota kama naweza kuwa waziri mkuu na hakuna mtu yeyote aliyejua mpango huo,kwani hakuna habari zilizovuja kabla,” anasema.

Alisema siku hiyo,akiwa nyumbani kwake amejipumzisha,alipata taarifa za kuitwa Ikulu na Rais Mkapa.‘‘Wala sikutegemea habari ya kuwa waziri mkuu,maana hata Mkapa mwenyewe sikuwa nimezoeana naye,”alisema.
Bofya na endelea>>>>>

No comments: